Katika vitu ambavyo vinawasumbua watu wengi wa maisha ya chini, kati na juu ni kuwa na tumbo kubwa yani kitambi ama kifriza kama wengi wanavyopenda kukiita.
Watu wengi hususani wanaume wamekua wakiongoza kwa kuwa na vitambi ambavyo husababishwa na aina ya vyakula vyenye sukari na mafuta mengi, ambavyo watu wengi huvipendelea kula mara kwa mara, kama ice cream, mikate, keki, chipsi, soseji, nyama, mayai na vyakula vingine vyenye lehemu na carbon kwa wingi.
Madaktari na wanasayansi wa afya ya binadamu wametoa njia mbadala na rahisi ya kupunguza tumbo na kuondoa kitambi ambacho ni mafuta yaliyojijaza kwenye sehemu ya misuli ya tumbo, njia hiyo bora, nyepesi, rahisi na isiyo na gharama ni ya unywaji wa maji kwa wingi kila siku.
Mwanadamu anatakiwa kwa uchache sana anywe lita tano za maji kwa siku, lakini kiwango ambacho ni kizuri na kinachohitajika ni lita saba, maji haya hutumika mwilini katika mifumo tofauti ya ufanyaji kazi wa mwili kama katika kumeng’enya chakula, kuweka ngozi kuwa laini na nyororo, kupunguza uzito na kuondoa mafuta mwilini, lakini pia kupunguza na kuondoa sumu mwilini, Lakini pia maji husaidia kuuweka mwili katika hali ya uchangamfu na wanasaikolojia wamesema maji husaidia kupunguza msongo wa mawazo na humsaidia mtu kutokua na hasira ovyo bila sababu.
Dr.-Oz1
Dr. Mehmet Oz.
Dr. Mehmet Oz kutoka hospitali ya Presbyterian nchini Marekani anafafanua na kukazia zaidi juu ya suala la unywaji wa maji na umuhimu wake kwa binadamu.“mahitaji ya maji yanatofautiana kati ya mtu na mtu. Mambo kama jinsia, hali ya hewa, kiwango cha joto la mwili, ushiriki wa mazoezi, aina ya kazi, umri na aina yam lo unaokula ni mambo yanayotakiwa kuzingatiwa”.
 Imeandaliwa na Hashim Ibrahim
Kitambii