Postedy by Esta Malibiche on August 9.2016 in KITAIFA with No comment
WAZIRI wa mambo ya ndani ya Nchi,Mwigulu Nchemba ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuweachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na vitendo vya kibaguzi baina ya wakimbizi
Akizungumza katika kambi ya wakimbizi ya katumba mkoani katavi mapema leo hii wakati akifanya ukaguzi na kuhakiki katika kambi hiyo alisema kuwa Tanzania hatua tabia za
kibaguzi,moja kati ya sifa kubwa ya nchi yetu ni kushinda vita dhidi ya
ubaguzi wa aina yoyote tangu tulipopata uhuru.
Zoezi hiilo la uhakiki limefanyika ,kutokana na kuwepo kwa taarifa za baadhi yawakimbizi waliopo katika kambi hizo kujihusisha na watu waovu,,kufanya vitendo vya kibaguzi,
na kutoka nje ya kambi zao kwenda nchi jirani bila kibali.
Aidha Mbali na kambi ya katumba,pia alitembelea kambi ya Mishamo.Pia aliviagiza
vyombo vya usalama na kupitia serikali za mitaa kuwachukulia hatua watu
wanaojihusisha na vitendo hivyo.
'''''Natoa rai kwa raia wote tuliowapa kibali cha kufanya kazi,kuishi na
kuwa raia wa nchi yetu, waache kujihusisha na vitendo viovu na
vyakibaguzi.Hatutawavumilia watu ambao tumewakaribisha kwa nia njema
hapa nchini na baadae wahatarishe usalama na amani ya nchi yetu.'''''alisema Mwigulu
"usalama wetu,jukumu letu sote"
Add caption |
Picha na Festo Sanga |
0 maoni:
Chapisha Maoni