“Kuna uhutaji wa kuboresha vituo vya afya katika Wilaya zetu ili kupunguza msongamano wa wagonjwa wanao kimbilia katika hospitali kubwa kutafuta hudama ambazo zina wezekana kabisa kutatatuliwa na Zahanati na  vituo vya Afya ndani ya Wilaya”.
Hayo yalisemwa leo Agosti 9.2016  na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati wa ziara maalum ya kukagua Zahanati na Vituo ndani ya Jimbo la Segerea linaloongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo, Mh. Bona Kalua.
Dk. Kigwangalla aliiungana na Mbunge wa Jimbo hilo, Bi. Bona Kalua, Mkurugenzi Mtendaji  wa  Serikali Mhe.  Msongela Mitu Palela pamoja na viongozi wengine wa serikali  na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ilala.
Aidha,  Dk. Kigwangalla ameweza kushuhudia mapungufu mbalimbali katika Zahanati  ya  Segerea, Tabata A pamoja na  kituo cha Afya cha Mnyamani  ambapo amesema kuwa licha ya uwepo wao bado wanashindwa kuondoa suluhisho la foleni na msongamano katika Hospitali kubwa za Mkoa ambazo kwa sasa ni pamoja na Hospitali ya Amana ama Mwananyamala au Temeke kutokana na kukosa vyumba vya upasuaji hata ule mdogo.
“Msongamano wa wagonjwa Hospitali ya Amana tunaweza kupunguza tu endapo changamoto kubwa na  ukosefu wa Maabara, vifaa vya kutosha pamoja na uwepo wa chumba cha upasuaji. Hivyo naagiza kwenye Zahanati hizi zote kuhakikisha zinajenga Vyumba hivyo vya Upasuaji haraka na ndani ya miezi sita nitarejea kukagua tena kama mumeweza kutimiza maagizo yangu ama la” alisema Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo hayo.
Kwa upande wake, Dk. Rumishael Mwanga ambaye ni Mganga Mkuu wa Zahanati ya Segerea alieleza kwamba amekua akikabiliana na changamoto ya chumba cha upasuaji hivyo kwa maagizo hayo watayafanyia kazi.
“Wanapokuja wagonjwa wenye uhitaji wa operation kubwa hua tuna waandikia waende hospitali ya Amana kutokana na ukosefu wa chumba cha upasuaji” alisema Dk. Mwanga.
Aidha katika tukio la kutembelea kituo cha Afya cha Mnyamani, Dk. Kigwangalla  kuongezwa kwa vitanda vya wagonjwa pamoja na kupunguza watumishi wanaozidi na kuwapeleka kwenye vituo vilivyo pungukiwa watumishi wa kada hiyo.
Hata ivyo katika kituo cha afya cha Tabata A pamoja na Mnyamani kumejitokeza suala la migogoro ya maeneo na kupelekea vituo hivyo kushindwa kupanuliwa kutokana na kua na wakazi katika maeneo yao.  Mganga Mkuu Mfawishi Modesta Mwinuka katika kituo cha afya cha Tabata A amesema kwamba eneo la kituo hicho ni dogo na lina itaji kupanuliwa ilikuruhusu utanuzi wa kituo hicho.
“kituo chetu kina kabiliwa na kua na eneo dogo na eneo tuna lo litaka ambalo ni nje ya kituo chetu lipo chini ya mtu ambae ana taka kupewa kiwanja kingine ndo atuchie eneo hivyo inakua ni changamoto kwetu” alisema Dr. Mwinuka
Dk. Kigwangalla, ametoa pongezi za dhati kwa vituo vyote kwani vime weza kujitaidi katika upande wa usafi, kuwepo kwa watumishi, uwajibikaji wa watumishi na ubora wa majengo wa vituo hivyo licha ya mapungufu katika upande wa maabara na chumba cha upasuaji.
DSC_4664Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa katika Zahanati ya Tabata ‘A’ wakati wa ziara hiyo mapema leo Agosti 9.2016.