Jumatano, 3 Agosti 2016
Mazoezi 6 rahisi kufanya yenye tija mwilini
07:05
No comments
Wapo
watu wengi sana ambao si wanamazoezi au wanamichezo na hawajapata
fursa au muda stahiki wa kufanya mazoezi ya nguvu na wanahitaji kufanya
mazoezi kwa ajili ya kuiweka miili yao vizuri na kuimarisha afya zao na
pia wapate muonekano mzuri wanapovaa nguo zao.
Lakini
wanakutana na changamoto mbalimbali za kimaisha zinazowafanya washindwe
kutenga muda mrefu zaidi katika kufanya mazoezi, hata hivyo si lazima
mtu apoteze muda mrefu akifanya mazoezi ili apate mabadiliko chanya
katika mwili wake, zipo njia mbadala na rahisi ambazo mtu huweza
kuzitumia ili kufikia malengo anayoyaazimia.
Yafuatayo
ni mazoezi marahisi ambayo mtu huweza kuyafanya kila siku na akapata
mabadiliko chanya katika mwili, mazoezi haya yana tija nyingi ambazo mtu
akiyafanya kiufasaha zaidi huweza kupata mabadiliko ya haraka katika
mwili wake .
Azimio
kubwa la hili andiko ni suala la mazoezi na orodha ya mazoezi hapo
chini itamsadia mtu kupata mabadiliko ya kimwili kulinganana tofauti ya
kibayolojia na kimazingira ya mtu mwenyewe.
1.Kutembea
Kutembea
ni suala rahisi mno lakini ni kitendo chenye nguvu na tija mwilini,
kutembea husaidia kupunguza kiwango cha cholesterol mwilini, kukomaza
mifupa, kuweka mapigo ya moyo sawa, kuleta uchangamfu, kushusha chini
hatari na uwezekani wa kupata magonjwa mbalimbali kama kisukari na
ugonjwa wa moyo. Kitendo cha kutembea kwa dakika 60 kwa siku ni zoezi
tosha kwa mwili kwa bindamu.
2.Kuogelea
Kwa
lugha rahisi kuogelea huitwa zoezi kamili, maji husaidia kunyoosha
viungo ambavyo vimelegea na vina maumivu kutokana na kutofanya mazoezi
kwa muda mrefu, tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa kuogelea kunaboresha
hali ya akili na kumfanya mtu awe katika hali ya uchangamfu. Na
kupunguza kalori mwilini.
3.Squats
Zoezi
hili ni zuri katika kupunguza kalori mwilini kwasababu linahusisha
misuli mingi zaidi katika ufanyaji wake. Zoezi hili hufanywa kwa mfumo
wa kuchuchumaa ama kukaa na kusimama kwa awamu na mizunguko mingi
(reps).
4.Push –ups ( pushapu)
Dhamira
kuu la hili zoezi ni kukaza mwili eneo la juu, kati na chini kwa wakati
mmoja, mtu huweza piga push up 15 hadi 20 kwa wakati mmoja.
5.Kukimbia
Mtu
uweza kukimbia kwa dakika 30 au 45 ama zaidi mfululizo bila kusimama
kwa kasi tofauti, kukimbia huchangamsha akili, mwili na husaidia
kupunguza mafuta mwilini pamoja na kukomaza misuli na mifupa mwilini.
6.Inama – inuka (bent-over row)
Zoezi
hili huonekana rahisi kutokana na jina lake na mazoea ya watu kuinama
na kuinuka katika vitendo ama kazi mbalimbali za kila siku lakini mtu
anapofanya mara nyingi kwa wakati mmoja huwa zoezi tosha la kuuweka
mgongo, miguu, tumbo na shingo katika hali nzuri ya kujinyoosha.
0 maoni:
Chapisha Maoni