Postedy by Esta Malibiche on
Singida
HALMASHAURI
ya wilaya ya Singida, imekusanya mapato ya zaidi ya shilingi 18.3
bilioni, kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya mapato kati ya julai
mwaka jana na juni mwaka huu.
Makusanyo hayo ni sawa na asilimia 87 ya lengo la kukusanya shilingi 21,475,625,995,kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Hayo
yamo kwenye taarifa ya mweka hazina wa halmashauri hiyo, Raphael
Ngwijo,iliyowasilishwa mbele ya kikao cha kawaida cha baraza la madiwani
kilichofanyika mjini hapa.
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Singida, Rashidi Bandoa,akitoa
nasaha zake kwenye ufunguzi wa kikao cha kawaida cha madiwani wa
halmashauri hiyo kilichofanyika mjini Singida.Wa pili kulia (waliokaa)
ni Mwenyekiti wa halmashauri hiyo na diwani wa kata ya Msange, Elia
Digha na wa kwanza kushoto, ni Makamu Mwenyekiti na diwani wa kata ya
Makuro, Omari Mande.
Alisema
kati ya makusanyo hayo zaidi ya shilingi 543 milioni sawa na asilimia
64 ya lengo la kukusanya shilingi 842.7 milioni kutoka kwenye vyanzo
vyake vya mapato ya ndani.
“Kwa
upande wa ruzuku inayotolewa na serikali kuu kwa ajili ya kufidia kodi
na ushuru uliofutwa,tumepokea zaidi ya shilingi 64.9 milioni tu sawa na
asilimia 22 ya lengo la kupokea ruzuku ya zaidi ya shilingi 300
milioni”,alisema.
Aidha,Ngwijo
alisema serikali kuu pia imewapatia zaidi ya shilingi 13.2 bilioni kwa
ajili ya kulipia mishahara ya watumishi wa umma ambayo ni sawa na
asilimia 94 ya lengo la kupokea shilingi 14.2 bilioni kwa mwaka wa fedha
wa 2015/2016.
Mkuu
wa wilaya ya Singida,Elias Tarimo, akizungumza kwenye kikao cha kawaida
cha baraza la madiwani leo (02/8/2016).Dc Tarimo,amewaagiza madiwani
hao kusimamia dhana ya ‘Hapa ni Kazi Tu’,ili wilaya hiyo iweze kupaa
kimaendeleo.
Diwani
wa kata ya Ikhanoda wilaya ya Singida,Higa Mnyawi,akichangia kwenye
kikao cha kawaida cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya
Singida kilichofanyika mjini humo.
Baadhi
ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida,wakifuatilia kikao cha
kawaida cha madiwani kilichgofanyika mjini humo.(Picha na Nathaniel
Limu).
0 maoni:
Chapisha Maoni