Postedy by Esta Malibiche on August 10.2016 in BIASHARA
Mkurugenzi
wa kamapuni ya Kibogoyo ya jijini Dar es Salaam, inayojihusisha na
usambazaji wa vinywaji vya TBL,Jackson Mtei (katikati) akijaribu
kuwasha pikipiki yake ya matairi matatu aina ya Toyo, huku Mkurugenzi
wa Mauzo na Usambazaji wa TBL Group Gareth Jones (Kushoto)
akimshangilia wakati alipoibuka mshindi kwa kuvuka malengo ya usambazaji
wa vinywaji vya kampuni hiyo. kulia ni Meneja wa Mauzo na
Usamabazaji na TBL Group Kanda ya Kusini ,James Bokella, wakati wa
hafla iliyofanyia katika kituo cha mauzo cha Ubungo .
Mkurugenzi
wa Mauzo na Usamabazaji wa TBL Group Gareth Jones (Kushoto)
akimkabidhi Mkurugenzi wa kampuni ya Rassam ya Banana Ukonga jijini Dar
Es Salaam, Mwita Magaiwa Ufunguo wa pikipiki ya matairi Matatu aina
Toyo, mara baada ya kuibuka mshindi kwa kuvuka malengo ya usambazaji wa
vinywaji vya kampuni hiyo. Kulia ni Meneja wa Mauzo na Usamabazaji na
TBL Group Kanda ya Kusini ,James Bokella. Hafla hiyo iliyofanyia
katika kituo cha mauzo cha Ubungo .
……………………………………………………………………………………………………
Mawakala watatu wa kampuni ya
TBL Group wanaofanyia biashara zao jijini Dar es Salaam wamejishindia
pikipiki za usambazaji aina ya Toyo kila moja ikiwa na thamani ya
shilingi milioni 3.9 baada ya kuibuka washindi katika kampeni ya mauzo
ambayo ilikuwa inaendeshwa na kampuni kuanzia Mwezi Mei mwaka huu.
Hafla ya kukabidhi pikipiki hizo
za kubebea mizigo imefanyika katika kituo cha mauzo cha TBL Group cha
Ubungo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wateja na maofisa
mbalimbali kutoka kampuni hiyo.
Akiongea wakati wa kukabidhi
zawadi hizo,Mkuu wa kituo cha Mauzo na Usambazi wa TBL kanda ya
Kusini,James Bokella,alisema kuwa kampeni hiyo iliyolenga kuwawezesha
mawakala wadogo wa kampuni hiyo imefanyika kwa kipindi cha miezi mitatu
na kuwashirikisha wafanyabiashara 117 ambapo miongoni mwao watatu
wamevuka lengo la mauzo lililokuwa limewekwa na kampuni na wamefanikiwa
kujishindia pikipiki za kubeba mizigo aina ya Toyo.
Aliwataka wafanyabiashara hao kuwa
ni Rasam Traders wa Ukonga,Kupata Kuna Mungu Shop wa Mbagala na
Kibongoto Investment wa Sinza “Wafanyabiashara hao wamefanya vizuri
katika kipindi cha kampeni ya kuvuka lengo la mauzo ambalo kampuni
ilipanga na leo wanakabidhiwa pikipiki za kubebea mizigo kwa ajili ya
kuwarahishia shughuli zao za biashara hususani usambazaji wa
vinywaji”.Alisema Bokella.
Aliongeza kuwa kampeni hii ni
mwendelezo wa promosheni za kampuni kupitia mpango wa kuwaendeleza
wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa zake na mbali na kuwapatia zawadi
pia imekuwa na utaratibu wa kuwapatia mafunzo mbalimbali kwa ajili ya
kukuza biashara zao ambapo wamekuwa wakipatiwa mafunzo ya
ujasiriamali,utunzaji wa vitabu vya fedha,matumizi mazuri ya fedha
zao,usafi katika maeneo yao ya biashara na kanuni na sharia za kufanya
biashara nchini.
Alisema kampuni hiyo maarufu kama
Retail Development Programme imepata mafanikio makubwa kwa kuwafikia
wafanyabiashara wengi wanaosambaza bidhaa za kampuni na hivi sasa
biashara zao zimeimarika zaidi na mitaji yao kuongezeka na kuwafanya
waishi maisha bora pamoja na familia zao.
Baadhi ya wafanyabiashara
walioibuka washindi katika kampeni hii wameishukuru kampuni ya TBL Group
kwa kubuni promosheni zenye mwelekeo wa kuboresha maisha ya wateja wake
“Ninayo furaha kujishindia pikipiki ya kusambazia vijana,ushindi huu
unadhihirisha kuwa tunafanya kazi na kampuni inayotujali wateja
wake”.Alisema mmoja wa washindi Mwita Magaiwa anayemiliki biashara ya
Rasam Traders.
Mshindi Mwingine Jackson Mushi
mmiliki wa Kibongoto Investment amesema kuwa inatia moyo kuona
wawekezaji wakubwa kama TBL wanabuni mikakati ya kukuza wafanyabiashara
wadogo kama ambavyo wametoa pikipiki za kusambazia vinywaji “Zawadi hii
zinazidi kutupa motisha ya kufanya kazi kwa bidi”.Alisema
0 maoni:
Chapisha Maoni