Kwa mujibu wa wataalamu wa afya maji moto yanatibu magonjwa mengi ikiwemo: Figo, kutoa sumu mwilini, kuyeyusha mafuta tumboni, kurahisisha mzunguko wa damu, kuondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.
Maji ya moto yanatajwa kuwa na manufaa zaidi kuliko maji ya baridi. Wataalamu wa afya wanasema yanasaidia uyeyushaji wa chakula, yanazilinda figo na ogani muhimu mwilini.
Kuna tiba nyingi za kitabibu, zilizogawanyikaa katika makundi
mbalimbali. Kuna zile za hospitali ambazo ni lazima zinunuliwe, lakini
kuna tiba ambazo kwa ushauri wa daktari hata wewe unaweza kuziandaa bila
kutumia gharama kubwa.
Moja ya tiba hizo ni kunywa maji ya moto. Kwa
mujibu wa wataalamu wa afya maji moto yanatibu magonjwa mengi ikiwemo:
Figo, kutoa sumu mwilini, kuyeyusha mafuta tumboni, kurahisisha mzunguko
wa damu, kuondoa sumu kwenye ubongo na kusafisha haja ndogo.
Kunywa maji ya moto kila unapotaka kwenda kufanya
kazi ya nguvu au mazoezi iwe kama kinga na inashauriwa kila siku anywe
glasi nane ili kutoa taka na kila kisichotakiwa kubaki mwilini, kupitia
jasho.
Wadau wa afya wanasema kuwa ni vyema pia kunywa
maji ya moto yenye ndimu au limao kabla ya kifungua kinywa ili
kurahisisha mfumo wa mwili kwa siku nzima.
Pazi Mwinyimvua, Mtaalamu wa Chakula na Lishe
kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anasema kuwa maji yanarahisisha
uyeyushaji wa chakula na mafuta mwilini, hivyo kutokana na umuhimu huo
ni vyema kunywa maji ya moto yatakayofanya kazi haraka na kwa ufanisi
mkubwa bila kuchosha figo.
Anaitaja faida nyingine ya kunywa maji ya moto
kuwa ni kutoa sumu zilizopo kwenye mishipa ya fahamu na kuisaidia figo
kufanya kazi kikamilifu, tofauti na maji baridi ambayo yanagandisha na
kuilazimisha figo kuyeyusha kwanza na kisha kuchuja
Anashauri umuhimu wa kunywa maji moto kabla ya
kufanya mazoezi kuwa ni kujiandaa kwa ajili ya kuchuja jasho ambalo
litatoa sumu, hivyo yakiwa ya moto yakifika yanaanza kufanya kazi moja
kwa moja, kuliko yakiwa ya baridi yanaweza kusumbua kwa kuwa ni lazima
yapate joto la mwili kwanza kabla ya kuanza kufanya kazi.
“Ukiachilia kusubiri yachemke pia ni kumuepusha
mtumiaji na hatari ya kuumwa tumbo kutokana na kunywa maji ya baridi
bila kuweka kitu tumboni na kwenda kufanya mazoezi kitu kinachoweza
kuzidisha maumivu au maji kucheza wakati wa kukimbia kama mazoezi ya
kukimbia. Lakini yakiwa ya moto ni kama umekunywa chai au kula chakula
cha kawaida” anasema Mwinyimvua.
Mwinyimvua anaongeza kuwa maji ya moto ni mazuri
hata kwa kupata choo, kwa vile kinarahisisha uyeyushaji na uchambuaji wa
kinachotakiwa na kisichotakiwa, wanaokunywa ya baridi wana uwezekanao
mkubwa wa kupata haja kubwa kwa shida.
Vilevile Mwinyimvua anashauri kuwa ni vyema kunywa
maji moto yaliyochemshwa na kuyaacha yapoe na kuwa vuguvugu na kuongeza
limao na asali mbali na kuongeza ladha, asali na limao vina faida
kiafya.
Gayl Canfield , RD, Mkurugenzi wa Lishe kutoka
katika Kituo cha Biashara cha Pritikin Longevity kwenye Mji wa Miami ,
Florida nchini Marekani, anasema kuwa kunywa maji ya uvuguvugu au ya
moto ni vyema kwa kuwa hufanya kazi moja kwa moja kutokana na hali ya
tumbo kuwa na joto muda wote.
Canfield anasisitiza, “Maji ni muhimu kwa mwili
wako, yakiwa ya moto ni bora zaidi, kwa kuwa yanatoa rangi ya njano
ya mkojo na kuufanya uwe msafi na wenye rangi angavu”.
Anasema maji ya moto yanaweza kukusaidia kupoteza uzito au kudumisha uzito ulionao sasa.
“Maji ya moto yanaweza kuongeza joto la mwili na
hivyo kuongeza kiwango ufanyaji kazi wa mwili kidogo, “ anasema Dk
Michael Wald , Mkurugenzi wa Huduma za lishe katika kituo cha Integrated
kilichopo New York, Marekani.
Anasema ili mwili ufanye kazi ipasavyo husaidia
utumbo na figo kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Kunywa maji ya moto pia
husaidia kupunguza uzito wa mwili na kuwa na nuru na siyo kusinyaa.
Vilevile huchangamsha utendaji kazi wa ubongo.
Dk Michael Wald anaitaja faida nyingine ya
kunywa maji ya moto kuwa ni kujenga mazoea ya kuchemsha maji hivyo
kupunguza idadi ya maambukizi yanayotokana na kunywa maji bila
kuchemsha.
“Maji baridi hugandisha mafuta ndani ya miili
yetu, ikiwa ni pamoja na mishipa ya damu,hali hii ikiendelea inaweza
kusababisha shinikizo la damu kutokana na ukosefu wa mzunguko wa damu
pamoja na magonjwa mengine mengi. Kama haikufanyiwa kazi inaweza hata
kusababisha saratani ” anasema Dr Michael Wald .
Mganga Mkuu Hospitali ya Amana, Dk. Meshack
Shimwela, anasema kuwa kunywa maji ni muhimu yawe baridi au ya moto na
hakuna sababu za kitaalamu zinazohusisha na dawa au kutibu kitu
chochote.
Anasema, watu wa tiba mbadala ndiyo wamelikuza
hilo lakini kitaalamu halipo na kunywa maji ni muhimu kwa kila mtu bila
kujali ni ya moto au baridi, hayo mengine ni maneno tu.
“Watu wanashauriwa kunywa maji ya moto kwa wale
wasiopenda kunywa maji, kwa kuwa yakiwa ya uvuguvugu inakuwa nafuu kwao
kunywa na wengine huambiwa waweke ndimu au limao siyo kama dawa bali
kuyapa ladha ili waweze kunywa” anasema Shimwela.
Anaendelea kufafanua kuwa kama kuna wanaodharau
kunywa maji wakiona ni kitu kidogo wanakosea sana kwa kuwa maji ni
msaada hata unapopata tatizo la kiafya.
Anasema kuwa hata katika usagaji wa chakula maji husaidia, hivyo kama mhusika amekunywa maji atarahisisha kitendo hicho.
Dk Raymond Mwenesano wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili, anasema kuwa kunywa maji ni muhimu kwa kila mwanadamu ili
kurahisisha utendaji wa mwili ikiwamo mzunguko wa damu bila kujali ni
moto au baridi.
Dk Mwenesano anazitaja faida za kunywa maji moto
kuwa ni : Kuboresha uyeyushwaji wa chakula. Maji ya vuguvugu yakiwekwa
limao, yanasaidia usafishaji wa tumbo, kuondoa sumu mwilini kupitia
jasho, kusafisha pua na koo, kuboresha mzunguko wa damu , husaidia
upatikanaji wa haja kubwa, kuongeza kinga mwilini endapo asali na limao
vitaongezwa.
ZIJUE FAIDA ZA KUNYWA
MAJI YA MOTO/UVUGUVUGU
Kuboresha uyeyushwaji wa chakula. Maji ya vuguvugu yakiwekwa limao
,yanasaidia usafishaji wa tumbo
Kuondoa sumu mwilini kupitia jasho
Kunywa maji y a moto au uvuguvugu kunasaidia kusafisha pua na koo
Kuboresha mzunguko wa damu
Kuongeza kinga mwilini endapo asali na limao vitaongezwa
Husaidia upatikanaji wa haja kubwa
DOKEZO
Kunywa maji moto ni muhimu kwa afya.Jenga mazoea ya kunywa maji moto
mara tu baada ya kuamka kwa matokeo mazuri.
Usinywe maji moto kutoka katika bomba. Chemsha maji na yaache yapoe na
kuwa vuguvugu. Unaweza kuongeza asali au limao au vyote. Mbali na
kuongeza ladha, asali na limao vina faida kiafya
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
ZIJUE FAIDA ZA KUNYWA
MAJI YA MOTO/UVUGUVUGU
Kuboresha uyeyushwaji wa chakula. Maji ya vuguvugu yakiwekwa limao
,yanasaidia usafishaji wa tumbo
Kuondoa sumu mwilini kupitia jasho
Kunywa maji y a moto au uvuguvugu kunasaidia kusafisha pua na koo
Kuboresha mzunguko wa damu
Kuongeza kinga mwilini endapo asali na limao vitaongezwa
Husaidia upatikanaji wa haja kubwa
DOKEZO
Kunywa maji moto ni muhimu kwa afya.Jenga mazoea ya kunywa maji moto
mara tu baada ya kuamka kwa matokeo mazuri.
Usinywe maji moto kutoka katika bomba. Chemsha maji na yaache yapoe na
kuwa vuguvugu. Unaweza kuongeza asali au limao au vyote. Mbali na
kuongeza ladha, asali na limao vina faida kiafya
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ
0 maoni:
Chapisha Maoni