Katika
tukio ambalo limewashtua watu wengi, watoto 11 wanatajwa kupoteza
maisha baada ya kuungua moto wakati wakiwa katika moja ya hospitali
mjini Baghdad, Iraq.
Katika
taarifa imetolewa na Wizara ya Afya ya nchi hiyo, imesema kuwa
tukiohilo lilitokea usiku wa Jumanne baada ya kutokea mlipuko wa moto
katika chumba cha uzazi katika hospitali ya Yarmouk.
Baada
ya kutokea mlipuko huo, watoto tisa na wanawake 29 waliondolewa katika
hospitali hiyo na kupelekewa eneo lingine na taarifa zinaeleza kuwa
chanzo cha mlipuko huo ni matatizo ya umeme
0 maoni:
Chapisha Maoni