Postedy by Esta Malibiche On August 11.2016
Kamishna Jenerari wa Jeshi la
Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akichangia damu katika moja ya
matukio ya kijamii ambayo jeshi hilo limekuwa likishiriki.
………………………………………………………………………….
NA VICTOR MASANGU, PWANI
HOSPITALI teule ya rufaa ya Mkoa
Tumbi kwa sasa bado inakabikabili na changamoto ya upungufu wa damu
safi na salama hivyo kupelekea baadhi ya wagonjwa wengine wakiwemo
watoto wenye umri chini ya miaka mitano wakinamama wajawazito, pamoja
na majeruhi wa ajali za barabarani kushindwa kupatiwa huduma ya
matibabu kwa wakati muafaka.
Kufuatia kuwepo kwa changamoto
hiyo jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani limeamua kuendesha
zoezi maalimu kwa askari wake kwa ajili ya kuweza kujitolea kuchangia
damu ili kuokoa maisha ya watu wanaopoteza maisha yao kutokana na
upungufu wa damu.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo
la uchangia wa damu Mratibu wa kitengo cha damu katika hospitali ya
Tumbi Elisia Towo alisema kwamba kutokana na idadi ya wagonjwa kuwa ni
kubwa hivyo uhitaji ni mkubwa kwani kwa sasa wanatumia uniti 12 mpaka
20 kwa siku ambazo bado hazijitolelezi kwa wagonjwa.
“Kwa sasa katika hospitali ya
tumbi bado inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa kuwepo kwa damu safi na
salama, lakini kikubwa tunawashukuru uongozi wa jeshi la zimamoto na
uokoaji Mkoa wa Pwani kwa kuamua kuitolea na kuchangia damu katika
hospoitali yetu, kwa hivyo ninaomba na watu wananachi wengine wawe na
moyo wakujitolea katika kusaidia,”alisema Towo.
Aidha alisema kwamba hospitali
ya tumbi imekuwa ikipokea wagonjwa wengi hivyo kunahitajika kuwepo na
akiba ya uniti zaidi ya 3000 za damu kwa kipindi cha mwaka mmoja ili
kuweza kukidhi mahitaji ya wagonjwa wenye mahitaji.
Kwa upande wake Kamanda wa jeshi
la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani Gudluck Zelothe alisema kwamba
wameamua kuchangia damu katika hospitali ya Tumbi ili kuweza kuwasaidia
wagonjwa mbali mbali ambao baadhi yao wamekuwa wakipoteza maisha
kutokana na kukosa huduma ya damu hivyo wakaona ni vema askari wake
wajitolee ili kuweza kucangia.
Naye afisa uhusianao wa jeshi
la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Pwani Irison Mkonyi alisema nia yao
kubwa ni kuhakikisha wanaweka mipango mikakati ya kuwasaidia watu amnbao
wamekuwa wakipungikiwa damu kwa kuendesha zoezi la utoaji wa damu kwa
kila muda wa miezi mitatu lengo ikiwa ni kuokoa maisha ya Watanania.
Naye Mhamasishaji wa damu safi
na salama katika hospitali ya Tumbi Feliciana Mmasi amesema kwamba
watoto wadogo wenye umri chini ya miaka mitano pamoja na wakinamama
wajawazito wanahitaji sana huduma ya damu safi na salama ili kuweza
kuokoa maisha yao.
JESHI la zimamoto na uokoaji
Mkoani Pwani limeamua kuendesha zoezi la kujitolea kuchangia damu katika
hospitali teule ya rufaa Mkoa tumbi kwa lengo la kuweza kupunguza vifo
vinavyotokana na kukosa upatikanaji wa damu .
0 maoni:
Chapisha Maoni