Kocha wa zamani wa Chelsea ambeye kwa sasa anakinoa kikosi cha Bayern Munich, Carlo Ancelotti ameelezea maisha yake ya kazi na jambo la aibu lililomkuta wakati akiwa kocha wa timu Chelsea miaka sita iliyopita.
Akizungumza na mtandao wa FourFourTwo, Ancelotti alisema kuwa moja ya matukio ya aibu yaliyowahi kumtokea akiwa kocha wa Chelsea ni kufungwa mchezo wa robo fainali na Manchester United na kuwa na uwiano wa goli 3-1 na baada ya mchezo mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich akaingia katika chumba cha kubadilishia nguo cha wachezaji.
“Ilikuwa kawaida kwa mmiliki (Roman Abramovich) kuja katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo kumalizika,
“Lakini baada ya mchezo kila mtu alijihisi aibu, kulikuwa na ukimya, lakini nilivunja ukimya na kuanza kuzungumza,” alisema Ancelotti.
Hata hivyo baada ya kumalizika msimu, Mei 22, 2011 Chelsea ilitoa taarifa ya kumfukuza kazi kocha huyo.