Watu
wengi hupendelea kulala huku wakisikiliza muziki lakini wamekua
wakipatwa na changamoto mbalimbali kama ya kukosa vifaa, kwani
imezoeleka kua na spika kubwa, au spika ndogo za masikioni ambazo
zinawapa wakati mgumu sana pale wanapo lala au wanapokua na watu wengine
wasiokua na haja ya kusikiliza mziki huo.
Mtafiti
kutoka shirika la ZEEQ, Warrick Bell amebuni Mto wa kulalia wenye uwezo
wa kutoa mziki kwa sauti ndogo itakayoweza kukuburudisha mpaka ulale
bila kumsumbua mtu wa pembeni yako. Kwani sauti yake inatoka kwa atakae
ulalia tu.
Mto
huo ambao unauwezo wa kutoa muziki kutoka kwenye simu yako ya mkononi,
kompyuta au kutoka mtandaoni (online streaming). Pia unauwezo wa
kudhibiti muda wako wa kulala na kuamka kwa kutumia apps za simu yako.
“wazo
la kutengeneza mto huu lilitokea kwenye shida kubwa niliokua naipata
wakati nikitafuta usingizi huku nikisikiliza mziki bila kumsumbua mke
wangu na kuamua kuweka spika zisizo na waya ndani ya mto” alisema Bell.
ZEEQ,
ambayo kwa sasa imeweza kupata zaidi ya shilingi dola milioni 220,000$.
Katika mauzo yake ya kickstarter, inauwezo wa kutetema wakati mtu ana
koroma, ikiwa na lengo la kukushtua ili uweze kubadilisha jinsi ulivyo
lala.
Imeandikwa na Laudanus Majani
0 maoni:
Chapisha Maoni