Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene amezitaka halmashauri za wilaya nchini kuona uwezekano wa kuwatumia waendesha maguta -ama pikipiki za miguu mitatu kama njia ya kutengeneza ajira kwa vijana kupitia shughuli za usafi katika mitaa na miji.
Akizungumza katika zoezi la usafi wa kila mwisho wa mwezi aliloshiriki katika mji mdogo wa Vwawa mkoani Songwe, waziri Simbachawene amesema utaratibu uliobuniwa na mkuu wa mkoa wa Songwe Luteni mstaafu Chiku Galawa, utasaidia kupunguza gharama za usafi mijini huku wakijiri vijana.
Amesema kutokana na yale aliyojifunza mkoani Songwe,anaangalia uwezekano wa ofisi yake kuanzisha mashindano ya usafi kwa halmashauri za wilaya kila baada ya miezi mitatu hadi sita na washindi watatangazwa kitaifa, aidha mashindano hayo pia yatakuwa ngazi za mikoa
chanzo;mbeya yetu blog
0 maoni:
Chapisha Maoni