Balozi wa Jamuhuri ya
korea nchini Tanzania Song Geum Young amewataka watanzania kuunga mkono juhudi
za Mh. Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr.John Magufuli kwa vitendo kwa kufanya kazi kwa bidii ili Taifa liweze
kusonga mbele kimaendeleo na kuondokana na umasikini.
Kauli hiyo aliitoa
wakati akizungumza na wananchi cha kijiji cha Mtula kilichopo Halmashauri ya
Mufindi wakati wa kukabidhi taa ndogo za solar katika zahanati ya Mtula alipotembelea jimbo la Mafinga Mjini mkoani hapa, huku akiambatana na uongozi wa Shirika la World Share.
Balozi Young alisema
Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alisema uhuru ni kazi,watanzania wote
hawapaswi kusahau wosia huo na hatmae kuuenzi kwa kuwajibika katika kufanya kazi
kwa bidii kwa kuuenzi kwa vitendo ili kuendana na kasi ya Mh. Rais wa awamu ya
Tano Dr.Magufuli
‘’’’’’Kama Rais anasema
‘HAPA KAZI TU’ hatuna budi kumuunga mkono kwa vitendo juhudi zake kwa kutatua
baadhi ya changamoto zinazoiwakabili wananchi ,kwasababu serikali pekee haiwezi
kukamilisha kila kitu.Kwakutambua hilio nimeona niitikie ombi la Mbunge Chumi baada ya ombi lake la muda mrefu kuniomba kutembelea Jimboni kwake,nimekuja na sirika la world share katika ili kuona namna ambayo
tunaweza saidia ‘’’’’’alisema Balozi
Balozi Young katika ziara yake hiyo alitembela skimu ya
umwagiliaji iliyopo katika kijiji
cha Mtula inayoendesha na chama cha
Ushirika cha Mtula chenye wanachama 68 huku kaya 390 zikinufaika na Mradi huo .
Mbali
na kutembelea skimu ya umwagiliaji alikabidhi msaada taa 400 zinazotumia mionzi
ya jua katika shule ya Msingi makalala,Zahati
ya Mtula,na katika jiji cha Bumilainga
na Itimboa,pia alikabidhi mafuta maalumu kwa wananfunzi wenye ulemavu wa ngozi
albino waliopo katika shule ya Makalala.
‘’’’’’’’’’World Share hapa nchini Tanzania inatoa misaada mbalimbali ikiwemo ya uchimbaji
wa Visima, Ujenzi wa matenki na mifumo yote ya maji, kusadia watoto yatima na
watu wenye Albino Pamoja na kutoa msaada
wa taa zinazotumia sola kwa kaya masikini zisizokuwa na kipato cha kununua taa’’’’’’’’’
Kwa upande wake Mkuu wa
wilaya ya Mufindi Jamuhuri David Willium akizungumza na wananchi katika kijiji
cha Mtula wakati wa ziara ya Balozi wa Jamuhuri ya korea Nchini Tanzazia
aliwataka wananchi kuhakikisha wanadumisha Amani iliyopo pamoja na usalama wake ili Nchi
iendelee kuwa yenye Amani na utulivu
Jamuhuri aliwataka
wakulima kulima kwa bidii na kukitumia vizuri chakula na kuwa na akiba ili kukabiliana na tatizo la
njaa lisiweze kutokea wilayani humo
‘’’’’’Pamoja na hayo,
ninawaomba wazazi na walezi muhakikishe mnawapeleka watoto shule,na kwa wale
vinara wa kukwamisha masomo kwa wanafunzi wa kike kwa kuwapa mimba nawapa onyo,sitamvumilia mtu yeyote ndani ya
wilaya yangua atakaebainika na kukwamisha masomo kwa mtoto wa kike..Tufanye
kazi kwa bidii kama Mh.Rais alivyoagiza na tuwalinde watoto,hasa watoto wa kike ili wasiweze kukutwa na vitendo vya
unyanyasaji wa kijinsia ikiwemo kubakwa hali inayopelekea kukwamisha ndoto zao
za baadae.’’’’’’alisema Jamuhuri
Awali Mkuu wa shule ya
Msingi mchanyiko Makalala akisoma taarifa ya shule kwa balozi alizungumzia changamoto
ya uhaba wa Maji katika shule hiyo, mkuu
wa shule Shem Muheni alisema wanafunzi
hao wanapata mateso makubwa kukosa maji maji safi na salama ukizingatia wanafunzi
wanaosoma katika shule hiyo ni wale wenye ulemavu.
‘’’’’’Shule hii ina jumla ya wananfunzi 548 kayi ya 85
wana ulemavu tofautitofauti ukiwemo wa viungo,Ngozi albino,Vichwa vikubwa
pamoja na ulemavu wa akili.Tatizo kubwa jingine llinalowakabili wanafunzi hawa ni ukosefu wa mazingira rafiki
ya kusomea wanafunzi hao pamoja na uchakavu wa miundombinu ya Mabweni ‘’’’’’Muheni
Kwa Upande wake mbunge wa jimbo la Mafinga mijini Cosato
Chumi alimshukuru Blaozi kwa kukubali ombi lake na kutembelea jimboni hapo, ambapo alisema kuwa lengo la Balozi
kuja katika jimbo la Mji wa Mafinga ni kuangalia changamoto zinazolikabili
jimbo hilo ili kuona namna ya kutusaidia kutatua
Mbunge Chumi alimshukru
Balozi kwa msaada wa taa za solar alizozitoa katika shule ya Msingi n
Mchanganyiko Makalala,kwa wanakijiji pamoja na zahanati ya Mtula na kusema kuwa
zitasaidia wakati wa usiku mara soala
iliyopo itakapoleta shida ukizingatia zahananti hiyo bado haijafikiwa na umeme,pamo.
Hata hivyo akiwa katika mradi wa skimu ya umwagiliaji
uliopo nkatika kijiji cha Mtula aliwataka vijana kutumia skimu
ya umwagiliaji katika kilimo,na kuwaasa kuachana na tabia ya kukimbilia mjini
kutafuta ajira wakati fursa za kilimo zipo na ni ajira tosha ambapo wakikitumia vizuri kin kinaweza
kuwaingizia kipato na kujikwamua kimmaisha
MWISHOOOO
0 maoni:
Chapisha Maoni