Alhamisi, 4 Agosti 2016

Huduma ya usafiri wa Treni ya Pugu kutolewa bure mpaka Ijumaa Agosti 05, 2016

 Treni
ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) ikiwa tayari kwa safari yake
ya Jiji kuanzia Stesheni  kwenda Pugu huduma ambayo
imeanza kutolewa huku ikiwapa abiria nafasi ya kusafiri bure hadi Ijumaa Agosti 5, 2016 .
Taarifa kutoka makao makuu ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), inaeleza kuwa huduma ya treni ya Pugu itaendelea kuwa ya majaribio hadi Ijumaa Agosti 5, 2016. Hivyo ndiyo kusema abiria wataendelea kujinafasi kwa huduma hiyo ya bure hadi siku hiyo. 

Kuanza rasmi kwa huduma hiyo kutategemea idhini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na majini (Sumatra). Leo Jumatano Agosti 3, 2016 Wataalamu wa Sumatra walisafiri na treni hiyo na kutoa maagizo maalum ya kurekebisha mabehewa ya treni hiyo, na TRL imeshajiandaa kufanya marekebisho hayo kwa wakati muafaka.

0 maoni:

Chapisha Maoni