Jumatano, 3 Agosti 2016

CHAMA CHA MAPINDUZI CCM MKOA WA IRINGA CHAMUUNGA MKONO MWENYEKITI WA CCM TAIFA DKT.MAGUFULI

Postedy by Esta Malibiche on August 3.2016 in SIASA with No comment
Chama cha Mapinduzi ccm Mkoa  wa Iringa kinaungana na wanaccm Tazania kumpongeza Mwenyekiti Mpya Dkt. John Pombe Magufuli kwa kukubali kupokea kijiti kutoka kwa alikuwa Mwenyekiti wa ccm Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Wakizungumza na Mdandao huu wa KALI YA HABARI mapema leo hii  kwa nyakati tofauti,Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu alisema kuwa  wanaimani na Dkt .Magufuli kutokana na utendaji wake mahili wa kazi  wa kuhakikisha wanyonge wananufaika na rasilimali za nchi zilizopo nchini,hivyo ndani ya chama wanaimani kuwa ataweza kurudisha heshima ya ccm kwa wananchi.
‘’’’Tunategemea mabadiliko makubwa ndani ya ccm,kama tulivyooona mabadiliko ndani ya Serikali,hivyo ccm Iringa tunamuunga mkono Mh. Rais kwa juhudi zake,pia tunaahidi kumpa ushirikiano wa kutosha ndani ya chama ili kuiletea heshima ccm ’’’’’’alisema Msambatavangu
Nae katibu wa ccm Mkoa wa Iringa HASSAN Mtenga alisema kuwa hapo awali ccm ilipoteza mwelekeo na wananchi wakakosa tumaini kwa ccm,kwa sasa wananchi wamerejea kwa asilimia 100 kutokana na utendaji kazi wa Mwenyekiti Dkt.John Magufuli.
‘’Sisi kama wanaccm tunafarijika sana,kwa mkoa wa Iringa tunatoa pongezi za dhati kwamwenyekiti wa ccm Taifa na tunamuombea kwa mungu amzidishie Afya njema ili aweze kuendelea kuimarisha chama kwa kufuata nyao za waasisi na viongozi waliopita na waliopo ‘’’’alisema Mtenga
Akimzungumzia Mwenyekiti Mstaafu Dkt.Kikwete ,Katibu Mtenda alisema ,Dkt. Kikwete alikuwa karibu sana na watanzania wote bila kubagua vyama vyao na alitumikia chama na Taifa kwa ujumla  kwa kufungua njia  kwa vijana kupata fursa  za kutumikia Taifa  katika Nyanja mbalimbali,hivyo ni hazina kubwa ndani ya ccm.
Salim Asas ni kamanda wa vijana ccm Mkoa wa Iringa nae alisema kutokana na kasi ya utendaji kazi  wa Mwenyekiti Mpya wa ccm Dkt.John Magufuli anaamini ataweza kukifikisha chama mahali pazuri na kuleta heshima ndani tya ccm na nje kwa manufaa ya Taifa kwa ujumla
Asas alisema kuwa Imani ya wanaccm awaliyonayo kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa kutokana na utendaji wake ndani ya serikali,wanategemea kupata mabadiliko makubwa ndani ya ccm .
‘’’Kasi yake ya utendaji naamin itasambaratisha upinzani nchini,huu ni ukweli usiopingika kutokana na kazi kubwa  ambazo wapinzani hawana pa kuanzia.Wanaccm tunaungana nae na tutampa ushirikiano wa kutosha ili kuirejesha ccm katika mstari unaotakiwa’’’’’’alisema Asas
Kwa upande wake katibu wa ccm Wilaya ya Kilolo Clemence Mponzi aliongeza kuwa toka Dkt.Magufuli akabidhiwe uenyekiti na kuanza kazi za chama wananchi wilayani kilolo wamekuwa na Imani kubwa kwa ccm kutokana na utendaji kazi wa Mwenyekiti serikalini  na wamehamasika kujiunga na ccm
‘’’’Ushindi wa kura 2,398 alioupa Dkt.Magufuli kutoka kwa wajumbe unadhihirisha kwamba amekubalika ndani ya ccm ,kutokana na hali hiyo kupata mabadiliko makubwa kama alivyoahidi wakati anakabidhiwa madaraka ya kukitumikia chama.na tuna Imani naye pia tuanamuahidi kumpa ushirikiano.
MWISHOO

0 maoni:

Chapisha Maoni