MKUU wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza amewataka waumini wa dini ya
Kiislam kuendelea kuhubiri amani na upendo katika taifa la Tanzania hata baada
ya kumaliza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani .
Alisema kuwa jukumu la kudumisha amani na umoja miongoni mwa jamii ni jambo
muhimu na linapaswa kulindwa na kila mmoja kwani amani pekee ndioyo itachangia
kuletea maendeleo kwa mtu binafsi na taifa kwa ujumla.
Aidha Masenza aliwataka wananchi kuwa walinzi kwa taifa lao na
kutoa taarifa pindi wakiona kuna watu au mtu wenye nia mbaya ya kuvuruga amani
au kiashirio cha ugaidi katika maeneo wanayoishi ili serikali kupitia jeshi la
polisi kuweza kuwajibika kuzuia na kulinda hali itakayojitokeza.
“Palipo na upendo watu wanaweza kuitana na kula chakula pamoja,
lakini kutokana na upendo kwa wateja wake crdb wametuita hapa kwa pamoja hivyo
nawaomba sana sana waumini wote wajitolee kutoa taarifa yoyote ambayo
itaonekana amani yetu inataka kuteteleka” alisema
Alisema kuwa palipo na amani kila mwananchi ataishi kwa uhuru
zaidi kuliko kuonekana kuna viashiria vya uvunjifu wa amani ambapo waathirika
wakubwa ni wanawake na watoto na kuwataka kudumisha amani iliyopo nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa CRDB Kanda ya Iringa, Kisa Samweli
amesema lengo la benki kuandaa futari kwa wateja wake ni kuimarisha umoja na
wateja wao na kuwa tawi la Iringa limefikia mafanikio waliyojiwekea ikiwa ni
pamoja na kukuza uchumi wa Taifa.
Kisa alitoa rai kwa watanzania kutumia benki ya crdb katika kukopa kwa lengo la
kuongeza kipato kwa wakulima, wafanyakazi na wafababiashara wakubwa na wakati
ambao wanahitaji mikopo kuweza kujiendeleza kwa kuwa mikopo hiyo ina riba nafuu
kwa kila mwananchi mwenye uwezo wa kukopa.






0 maoni:
Chapisha Maoni