Posted by Esta Malibiche
on 6:37
in
KITAIFA
|
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempongeza Mufti wa Tanzania
Sheikh Aboubakar Zubeir bin Ali kwa juhudi zake za kuwaunganisha waislamu wote
na kupanua uwigo wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kutoa huduma za
kijamii na ameahidi kuwa serikali ya awamu ya tano itaunga mkono juhudi hizo.
Rais Magufuli
ameyasema hayo leo tarehe 06 Julai, 2016 wakati akihutubia Baraza la Eid
el-Fitr kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, lililofanyika kitaifa katika viwanja vya Karimejee Jijini Dar es
salaam.
Dkt. Magufuli
amesema kitendo cha kuwaunganisha waislamu wote katika Baraza la Eid el-Fitr kinafungua
ukurasa mpya na ni moja ya hatua muhimu za kuimarisha amani, umoja na
mshikamano miongoni mwa waislamu wa makundi mbalimbali pamoja na watanzania
wengine waisio waislamu.
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikhe Aboubakar
Zubeir wakati alipowasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la
Eid El fitri lililofanyika katika viwanja hivyo.
|
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi mara baada
ya kuwasili katika viwanja vya Karimjee kwa ajili ya Baraza la Eid El fitri.
Aidha Rais
Magufuli amezungumzia juhudi zinazofanywa na BAKWATA katika kuimarisha taasisi
zake zinazotoa huduma za kijamii na kulinda mali zake akisema serikali itahakikisha
mali zote za waislamu zinakuwa salama na kwamba wote waliodhulumu mali za
waislamu watazirejesha.
Awali akisoma
taarifa, Katibu Mkuu wa BAKWATA Alhaji Suleiman Said Lolila amesema BAKWATA
inakusudia kupanua huduma za kijamii kwa lengo la kuwahudumia wananchi ikiwemo
kujenga chuo kikuu Mkoani Dodoma na pia amempongeza Rais Magufuli kwa juhudi
zake za kuondoa umasikini huku akimtaka asikatishwe tamaa na wachache
watakaoudhika kwa kuguswa na hatua zinazochukuliwa.
Nae Mufti wa
Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali pamoja na kumshukuru Rais Magufuli kwa
kuongoza bila ubaguzi amewataka watanzania kuungana na juhudi za serikali
kupinga matendo maovu ikiwemo rushwa na ufisadi na pia amelaani ndoa za jinsia
moja akisema ni kinyume na maadili ya dini.
Baraza la Eid
el-Fitr pia limehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Rais Mstaafu wa
awamu ya pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, mabalozi na wabunge.
|
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Mufti Mkuu Sheikh Aboubakar Zubeir.
|
 |
| Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia katika
baraza hilo la Eid El fitri. |
 |
| Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na baadhi
ya waumini wa dini ya kiislamu mara baada ya kumaliza kuhutubia katika viwanja
vya karimjee jijini Dar es | | Salaam. | | | | | | | | | | |
0 maoni:
Chapisha Maoni