Serikali
imewataka Wakuu wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii nchini kufanya kazi kwa
kuzingatia weledi , kanuni, miongozo na taratibu zinazosimamia
uendeshaji wa vyuo hivyo ili kuiwezesha sekta hiyo kupiga hatua kwa
kuzalisha wataalam wenye sifa wanaokidhi matarajio ya wananchi.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali
watu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bw.Erasimus Rugarabamu wakati akifungua kikao kazi cha wakuu wa vyuo vya
Maendeleo ya Jamii kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi.Sihaba
Nkinga.
Bw.
Rugarabamu amewataka wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii kuendelea
kusimamia kwa umakini mkubwa wa Rasilimali za vyuo hivyo na kubainisha
kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua za kinidhamu na kisheria kwa mkuu
wa Chuo yeyote atakayeshindwa kuzingatia weledi , kanuni na taratibu
zinazosimamia uendeshaji wa vyuo hivyo.
”
Ninyi ndio wasimamizi wa uzalishaji wa wataalam wa Maendeleo ya Jamii
nchini, mnao wajibu wa kubadilisha fikra za wananchi na kuwa chachu ya
maendeleo, hakikisheni mnasimamia vizuri suala la udahili wa wanafunzi
kwa kuwa na wanafunzi wenye sifa.
Aidha,
amewataka wakuu hao wa vyuo kuhakikisha kuwa wanapiga vita kwa vitendo
udahili wa vyeti vya kughushi ( vyeti feki) akisisitiza kuwa Serikali
haitasita kuchukua hatua za kisheria na kinidhamu kwa Mkuu wa Chuo
yeyoye atakayehusika kwa namna moja au nyingine kusaidia udahili wa
wananfunzi wasio na sifa.
Ametoa
wito kwa wakuu na Wakuu wa taaluma wa vyuo hivyo kuwa makini katika
suala la udahili wa wanafunzi wanaojiunga katika fani ya maendeleo ya
jamii ili kuendelea kujenga heshima ya taaluma ya Maendeleo ya Jamii na
kutimiza matarajio ya kuwaletea maendeleo wananchi.
”
Hakikisheni mnaepuka maslahi binafsi katika usimamizi wa taaluma, suala
la vyeti feki lisiwe na nafasi katika vyuo vyetu, fanyeni kazi kwa
kuzingatia sheria ili tuendelee kutoa wahitimu bora” Amesisitiza
Rugarabamu.
Katika
hatua nyingine amewataka wakuu hao kuwa wabunifu ili vyuo
wanavyovisimamia viweze kuhimili soko la ushindani kutoka vyuo vingine
vya elimu ya Maendeleo ya jamiii hapa nchini ili vyuo chini ya wizara,
viweze kutekeleza majukumu kwa ufanisi na kuzalisha wataalam wanaokidhi
mahitaji ya soko.
”
Ili vyuo vyetu viendelee kuonekana lazima viweze kuhimili ushindani
kutoka katika vyuo vingine vinavyotoa taaluma kama hii, jambo hili
lazima tulifanye kwa nguvu ili tuendelee kuwa wazalishaji bora wa
wataalam wa elimu ya Maendeleo ya Jamii hapa nchini” Amesisitiza
Rugarabamu.
Aidha, ametoa wito kwa wakuu hao kusimamia vizuri rasilimali za fedha
Upimaji
wa Wazi (OPRAS) Amesema kuwa watumishi wote wa Serikali lazima wapimwe
utendaji kazi wao kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa na kusisitiza kuwa
jambo hilo ni lazima
Aidha,
amewataka Wakuu hao kuhakikisha kuwa wanavisimamia vyuo wanavyoviongoza
kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha kuwa wanawasilisha taarifa kuhusu
maendeleo ya vyuo vyao kwa lengo la kuiwezesha Serikali kuchukua hatua
za katika maeneo ambayo hayaendi vizuri kuviwezesha vyuo hivyo kupiga
hatua kitaaluma.
Awali
akizungumza kabla ya ufunguzi wa mkutano huo, Kaimu Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Jamii wa Wizara hiyo Bw. Enterberth Nyoni amesema kuwa
Mkutano huo ni muhimu sana kwa kuwa umewakutanisha wakuu wa Vyuo na
Makamu Wakuu wa Vyuo wanaozalisha Maafisa Maendeleo ya Jamii nchini
ambao huajiliwa na Serikali katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, taasisi
na Mashirika mbalimbali.
Amesema
kuwa kufanyika kwa mkutano huo kuna umuhimu mkubwa katika maendeleo ya
nchi kupitia mchango wa maafisa maendeleo ya jamii ambao husimamia
shughuli za maendeleo ya wananchi kuanzia ngazi ya kijiji, kata hadi
Taifa pia usimamizi na utoaji wa elimu kuhusu Haki za makundi mbalimbali
katika jamii.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii vilivyo
chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Bw.
Paschal Joseph Mahinyila amesema kuwa vyuo vya Maendeleo ya Jamii
vinaendelea kufanya kazi nzuri ya kuzalisha wataalam wa masuala ya
maendeleo ambao wamekua msaada kwa wananchi.
Amesema
kuwa Serikali inaendelea kuifanyia kazi changamoto ya uhaba na uchakavu
wa majengo inayovikabili baadhi ya vyuo vya maendeleo ya Jamii ili
viweze kudahili wanafunzi wengi zaidi na kuendelea kutoa elimu katika
mazingira bora.
Aidha,
amesema kuwa kupitia kikao kazi hicho changamoto ya Miongozo ya
uendeshaji itaweza kufanyiwa kazi ili vyuo vyote viweze kuzungumza lugha
moja na kutekeleza matakwa ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi
(NACTE) pamoja na kuviwezesha vyuo vingine vya maendeleo ya jamii
vilivyo chini ya wizara hiyo kuanza kutoa wahitimu wa shahada ya kwanza
kwa kujiunga na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru, Arusha.
Naye
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Rugemba, Mafinga mkoani Iringa Bi.
Santina Mbata akizungumzia mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi hicho
amesema kuwa kukutana kwa wakuu hao wa vyuo vya Maendeleo ya Jamii ni
fursa pekee inayowapa fursa ya kujadili masuala mbalimbali ya kisera,
kisheria, taratibu na miongozo mbalimbali inayosimamia vyuo hivyo.
Bi.Santina
ameeleza kuwa licha ya chuo anachokiongoza kukabiliwa na changamoto
mbalimbali Serikali inaendelea kukijengea uwezo ili kuhakikisha kuwa
kinaendelea kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake kwa kuendelea
kuwajengea uwezo wananchi wanaopata mafunzo kukabilina na changamoto
mbalimbali za maendeleo ya wananchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni