Rais
Obama atafupisha ziara yake katika mataifa ya kigeni na kwenda Dallas
wiki ijayo wakati mashambulizi ya risasi yaliyofanywa na kijana mweusi
ambaye ni mwanajeshi wa zamani aliyetia nia ya kuwauwa polisi wazungu.
Mauaji hayo yamesababisha miito ya haraka kuleta hali ya kuvumiliana nchini humo kutokana na matatizo ya kibaguzi.
Polisi
waligundua vifaa vya kutengenezea mabomu na silaha katika nyumba ya
kijana huyo Micah Johnson mwenye umri wa miaka 25, mkaazi wa eneo la
Dallas ambaye aliwapiga risasi polisi watano kabla ya kufariki katika
mapambano ya silaha na polisi.
Ikulu ya
Marekani ya White House imeondoa uwezekano wa mahusiano kati ya
mshambuliaji huyo mwenye silaha na makundi yanayotambulika ya kigaidi,
mahusiano katika ukurasa wake wa Facebook yanaelekeza katika makundi ya
wanaharakati wenye msimamo mkali ya Wamarekani weusi ambayo
yameorodheshwa kuwa ni makundi ya chuki nchini Marekani.
Akielezewa
na polisi kuwa ni mshambuliaji aliyeamua kutenda kitendo hicho peke
yake na hakuwa na rekodi ya uhalifu hapo nyuma , Johnson aliwaambia watu
waliokuwa wanafanya nae majadiliano kabla ya kufariki kwamba alitaka
kuwauwa polisi wazungu kwa kulipiza kisasi kutokana na kuuwawa kinyama
hivi karibuni kwa watu wawili weusi.
Maandamano ya amani
Mashambulizi
hayo jimboni Texas, ambayo yalizuka siku ya Alhamis usiku wakati wa
maandamano ya amani dhidi ya ukatili wa polisi, yanakuja katika wakati
wa hali ya kutafakari kuhusiana na matumizi ya silaha kwa ulinzi wa
amani kuelekea Wamarekani weusi.
Viongozi
wa harakati za Maisha ya Weusi ni muhimu wameshutumu mauaji hayo mjini
Dallas, huku wakiapa kuendelea na maandamano yaliyopangwa kufanyika
mwishoni mwa juma, huku makundi makubwa ya watu wakijikusanya usiku wa
Ijumaa mjini Atlanta Georgia na wengine wengi wakiwa nje ya Ikulu ya
Marekani White House.
Akihutubia
maelfu ya watu katika sala iliyofanyika kwa heshima ya maafisa wa
polisi waliouwawa, meya wa Dallas Mike Raswlings amewataka Wamarekani ,
kuimarisha hatua , kuponesha vidonda vya ubaguzi nchini humo.
Maandamano yataendelea
"Hatutajitenga
na ukweli uliopo kwamba sisi kama wakaazi wa mji, wa jimbo, na kama
taifa tunapambana na masuala ya kibaguzi," ameliambia kundi la watu
waliokusanyika.
Rawlings
amerudia ujumbe uliotolewa na rais Obama wakati taifa hilo linahangaika
kutokana na ghasia hizo za hivi karibuni: Kwamba maisha ya weusi ni
muhimu , na kama ilivyo kwa maisha ya wazungu, wale maafisa wa polisi.
"Tunapaswa kuongeza nguvu na kuyakabili masuala tata kwa njia nyingine," amesema Rawlings. "Na masuala ya kibaguzi yanautata."
Obama ,
ambaye ameamuru bendera zote zipepee nusu mlingoti katika majengo ya
serikali kwa muda wa siku tano, aliweka wazi kwamba ghasia dhidi ya
polisi, haziwezi kuhalalishwa kabisa."
Rais
alizungumzia mashambulizi hayo akiwa katika mji mkuu wa Poland, Warsaw ,
ambako alikuwa akihudhuria mkutano wa kilele wa NATO, na kuiita hali
hiyo , "inayojirudia na ya kukera."
Ikulu ya
Marekani imesema Obama atarejea nchini Marekani usiku ya Jumapili, siku
moja kabla ya muda wake wa safari kumalizika, na kwenda kuzuru Dallas
mapema wiki ijayo kwa mwaliko wa meya Rawlings.DW
0 maoni:
Chapisha Maoni