Ijumaa, 8 Julai 2016

MZEE MALECELA AMUOMBA MKUU WA MKOA WA DODOMA KUFUFUA ZAO LA ZABIBU



Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana wakisalimiana na Viongozi wa skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino wakati walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki.

Afisa Kilimo Wilaya ya Chamwino Ndg. Godfrey Mnyamale akiwasilisha taarifa ya mradi wa skimu ya Umwagiliaji wa zabibu ya Chinangali II kwa mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Mzee Malecela (hawapo pichani) wakati walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa skimu hiyo.

Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana (kushoto) changamoto zinazo didimiza kilimo cha Zabibu Dodoma na kumtaka kufanya kila awezalo kufufua zao hilo sambamba na kuondoa tatizo la njaa Dodoma wakati viongozi hao walipotembelea skimu ya Umwagiliaji wa zabibu ya Chinangali II mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akiahidi kufufua zao la zabibu Mkoani humo na kuondoa tatizo la njaa kwa kufufua skimu zote za umwagiliaji zinazolegalega na kukosa uongozi imara wakati akizungumza na viongozi wa skimu ya umwagiliaji wa Zao la zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino mwishoni mwa wiki.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana na Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakikagua mitambo ya kusukuma maji kwenye skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.(P.T)

0 maoni:

Chapisha Maoni