Kila ifikapo Julai, 11 ya kila mwaka dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya idadi ya watu duniani ambapo kwa mwaka huu takwimu zinaonyesha kuwa kwa sasa dunia ina watu zaidi ya Bilioni 7.4 ikiwa ni ongezeko la asiliia 1.07 kutoka mwaka 2015 ambao ulikuwa na watu Bilioni 7.3.
Idadi ya watu mara ya kwanza ilianza kuhesabiwa mwaka 1950 na kulikadiliwa kuwa dunia ina watu Bilioni 2.5 lakini pia kwa mujibu wa tafiti ambazo zimefanyika kwa kulinganisha na ongezeko la watu inaelezwa kuwa hadi kufikia mwaka 2050 dunia itakuwa na watu Bilioni 9.5 na hadi kufika mwaka 2100 kutakuwa na watu Bilioni 10.8.
Kutokana na takwimu za mwaka 2016, Mo Blog imekuandalia orodha ya nchi 10 ambazo zinatajwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani.
1. China – Bilioni 1.382
2. India – Bilioni 1.327
3. Marekani – Milioni 324
4. Indonesia – Milioni 260
5. Brazil – Milioni 209
6. Pakistan – Milioni 192
7. Nigeria – Milioni 187
8. Bangladesh – Milioni 162
9. Urusi – Milioni 143
10. Mexico – Milioni 128
Kwa upande wa nchi za Afrika Mashariki, (katika mabano ni nafasi ya dunia);
1. (24) Tanzania – Milioni 55
2. (29) Kenya – Milioni 47
3. (35) Uganda – Milioni 40
4. (75) Sudani Kusini – Milioni 12
5. (76) Rwanda – Milioni 11.8
6. (77) Burundi – Milioni 11.5