Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu wa pili kushoto akitoa maagizokwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai wa kwanza kulia
wakati alipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es
salaam.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) Dkt. Samuel Swai
wa kwanza kulia akifafanua jambo kwa Waziri wa Afya ,Maendeleo ya
jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati alipotembelea
wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam
Waziri
wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy
Mwalimu akiwajulia hali baadhi ya wagonjwa waliopo katika taasisi ya
Mifupa Muhimbili (MOI)alipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo leo
jijini Dar es salaam.
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya
jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu katikati akimfariji
mtoto Rahel Razaro wa kwanza kushoto aliyelazwa katika Taasisi ya Mifupa
Muhimbili(MOI) alipotembelea wagonjwa katika hospitali hiyo leo jijini
Dar es salaam na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Taasisi
hiyo Dkt. Samuel Swai.
……………………………………………………………………………………………………………..
Na Ally Daud-Maelezo
Serikali chini ya Wizara ya Afya
,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na Watoto imeitaka Taasisi ya Mifupa
Muhimbili(MOI) kuhudumia wagonjwa haraka iwezekanavyo ili kuondoa
msongamano wa wagonjwa hospitalini hapo na kuwaruhusu wakaendelee na
shughuli za kujenga taifa.
Akizungumza hayo alipotembelea
wagonjwa MOI Waziri wa Afya ,Maendeleo ya jamii, Jinsia , Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu aliwataka watumishi wa taasisi hiyo kuwahudumia
wagonjwa haraka iwezekanavyo ili kuwapa fursa ya kwenda kufanya
shughuli za kimaendeleo kwa ajili ya taifa.
“Mnatakiwa kuhudumia wagonjwa kwa
haraka na ufanisi mkubwa ili kuwasaidia watanzania kutotumia muda
mwingi wakiwa hospitalina na badala yake wapone waende wakaendelee na
shughuli zao za kujenga taifa kwa maendeleo ya Nchi yetu”alisema Mhe.
Ummy
Aidha Mhe. Ummy ameongeza kuwa
licha ya kuwa na changamoto zinazojitokeza hospitalini hapo Wizara ipo
bega kwa began a Taasisi hiyo kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa
wananchi chini ya kitengo hiko ili kufikia malengo ya milenia.
“Nafahamu kama kuna changamoto
zinazoikabili taasisi hii kama mlivyonieleza lakini tupo pamoja katika
kuziondoa na nyinyi hakikisheni mnafanya kazi kwa bidii ili kuondoa
malalamiko ya wananchi na kuleta huduma bora na kwa wakati” alisisitiza
Mhe. Ummy.
Mbali na hayo Mhe. Ummy ameitaka
taasisi hiyo kurudisha huduma ya kufanya upasuaji kwa wagonjwa siku za
jumamosi bila ya kukosa tena kwa haraka ili kupunguza mlundikano wa
wagonjwa kwenye taasisi hiyo.
Kwa upande wa Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji MOI Dkt. Samuel Swai amesema kuwa wamepokea agizo hilo na wapo
tayari kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya watanzania kwa haraka
na ubora zaidi.
“Tupo tayari kutekeleza agizo la
Mheshimiwa Waziri la kufanya kazi kwa bidii ili kuokoa maisha ya
watanzania kwa haraka na ataona matokeo mazuri kuanzia leo hii”
alisisitiza Dkt. Swai.
0 maoni:
Chapisha Maoni