Jumatano, 3 Agosti 2016

UMUHIMU WA LISHE BORA KWA MTOTO WA MWA KA 1-4

Postedy by Esta Malibiche onAugust 3.2016 in Afya with No cmomment


  Lishe mbaya kwa watoto husababiswa na ukosefu wa Elim na ufaham mzuri wa  vyakula  na lishe bora  wa wazazi,lakini kwa upande mwingine hali ya wazazi kutokujali watoto wao kwa sababu moja au nyingine pia huchangia tatizo hili.Mtoto kukosa  usingizi wakutosha au kushindwa kulala vizuri pia huchangiwa sana na njaa,mtoto asiposhiba vizuri hawezi kulala vizuri.Kelele,kumchelewesha mtoto kulala na kukosa ratiba ya mtoto kulala pia huchangia mtoto kukosa usingizi wakutosha.

Watoto wa mwaka mmoja adi mine(1-4)wanahitaji masaa 14 ya usingizi kila siku.wanatakiwa kupata usingizi wa mchana wa kati ya saa moja adi masaa matatu na nusu(1-3.5),usiku wanatakiwa kulala kati ya saa moja na saa tatu(1-3) na asubui  waamke kati ya saa kumi na mbili na saa mbili (12-2) Ni kosa kabisa mtoto kua macho baada ya saa tatu,endapo mtoto wako huwa macho baada ya saa tatu ni kiashirio kwamba anashida au tatizo Fulani.

Asilimia kubwa sana ya watoto hawapati mboga na matunda yakutosha katika lishe zao.Watoto wenye ukosefu wa  vitamin muhim,madini mwili,na aside mafuta za muhim (essential fatty acids) huwa na akili zilizozubaa na hawafanyi vizuri darasani na wana asili ya ukali,watoto wengine huwa na unene wa ziada ambao pia husababishwa na lishe mbaya,Lakini kubwa kabisa mtoto huyo hawezi kukua katika uwiano ulio sahihi.

Watoto wanapofikia umri wa kuanza kwenda madarasa ya awali ndio ule wakati ambao mtoto hurefuka na mwili wake huwa na nguvu nyingi,huu ndio wakati ambao wanaanza kujifunza kujitegemea na kutengeneza wasifu binafsi(personalities).Mtoto huanza kubagua chakula,na kuamua anapenda au apendi chakula kipi.
Watoto wanaobagua chakula huwa kwenye hatari kubwa ya kukosa virutubisho maalum vinavyoitajika kuwezesha ukuaji wao,kwani virutubisho hivyo huchangia ukuaji bora wa akili,mwili,na hata hisia.
Ukuaji sahihi wa mifupa na meno kwa watoto umekua ni changamoto kubwa  sana,kwani asilimia kubwa ya watoto hawapati vitamini muhim,madini mwili na asidi mafuta ya kutosha kuwezesha ukuaji wao.

0 maoni:

Chapisha Maoni