|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine
Mahiga (Mb.), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza
zoezi la makabidhiano ya madawati kutoka Jumuiya ya Mabohora iliyopo
hapa nchini, jumuiya hiyo imechangia jumla ya madawati 105 yenye thamani
ya shilingi milioni kumi. Hii ni katika kuiunga mkono Serikali kwenye
zoezi la kuchangia madawati nchi nzima lililo tangazwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Madawati
hayo yametengenezwa hapa nchini na Kampuni ya Jambo. Tukio hilo
lilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere uliopo jijini
Dar es Salaam. |
|
Makamu
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora, Mhe. Shehe Zainuddin Adamjee naye
akizungumza na waandishi wa habari kwenye makabidhiano ya madawati. |
|
Sehemu ya Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini Waziri Mahiga (hayupo pichani) |
|
Sehemu ya wawakilishi wa Jumuiya hiyo wakimsikiliza kwa makini Mhe. Waziri Mahiga |
|
Waziri Mahiga akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya dawati kati ya yaliyotolewa na Jumuiya ya Mabohora. Wizara itakabidhi madawati hayo kwa Mamlaka husika kwa ajili ya kusambazwa. |
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akiwa na
Viongozi Wakuu wa Jumuiya ya Mabohora nchini, Mhe. Shekh Tayabali
Hamzabhai ( (kushoto) na Shekh Zainuddin Adamjee, Makamu Mwenyekiti
(kulia) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi madawati.
0 maoni:
Chapisha Maoni