Jumanne, 12 Julai 2016

MBUNGE WA MUFINDI KUSINI MENDRAD KIGOLA ATATUA KERO YA MAJI JIMBONI KWAKE





MBUNGE wa jimbo la Mufindi Kusini Mkoani Iringa  Mendrad Kigola amesema tatizo la uhaba wa maji lililokuwa linazikabili  shule za msingi jimboni humo,linaendelea  kutatuliwa kwa kasi kubwa, ambapo kwa sasa amechimba visima  5 vyenye thamani ya Tsh.Mill.60 huku kila kisima kimoja kikigharimu kiasi cha Tsh.Mill 12 katika shule za Msingi zilizopo jimboni humo,ikiwa ni moja ya utekelezaji wa ahadi yake aliyoliyoitoa wakati wa kapeni za uchaguzi mkuu 2015,kuwa endapo atapewa ridhaa ya  kuwa mbunge atahakikisha shule za Msingi zilizopo jimboni humo zinapata maji safi na salama.
Akizungumza jana katika kijiji cha Kinegembasi Kata ya Itandula  wakati wa zoezi la uchimbaji kisima katika shule ya msingi kinegembasi likiendelea Mbunge Kigola alisema lengo la kuchimba visima hivyo katika shule za msingi ni kutaka kutatua kero ya ukosefu wa maji safi na salama  katika shuleni.Pia alisema maji hayo yatawanufaisha wananfunzi na jamii inayowazunguka kwa ujumla.
‘’’’’’Baada ya  kuona watoto wa shule za msingi wanahangaika namana ya kupata maji safi na salama nikaona nguvu zangu zielekee huko kuchimba visima,ambapo hadi sasa nimechimba visima vitano katika  shule za msingi zilizopo jimboni kwangu.Shule hizo ni Wangamaganga ,Ihangana twa,Lugema, Ikaning’ombe ,Pamoja na shule ya Msingi Kinegebasi ‘’’’’alisema Kigola
Kigola alisema jumla ya kata 16 zilizopo jimbo lai Mufindi Kusini kati yake , kata 14 zinanufaika na maji safi na salama,ambapo asilimia 65 ya wananchi wananufaika na maji hayo, ingawa bado kata 2 zenye chanagamoto ya uhaba wa maji kutokana na mazingira yake kuwa kame,ila anaendelea kupambana na kuhakikisha anatatua tatizo hilo.
Aidha Kigola alisema kwa muda wa miezi 6 amechimba visima 12  kama mbunge  kwa kushirikiana na wadau, amekarabati visima 43 viliyotokana na uchakavu.Pia alisema toka mwaka 2011 alipochaguliwa mpaka mwaka 2016 amechimba visima 28 kwa nguvu zake yeye mwenyewe kama mbunge bila mchango wa wananchi.ataendelea kupambana kuhakikisha kata ya Itandula na …..zenye ukame zinafikiwa na maji ili wananchi waondokane na kero hiyo na hatimae waweze kupata maji safi na salama
 Alisema kwa bajeti ya fedha 2016/17 serikali imetenga kiasi cha Tsh.1.56 Till.kwa ajili ya  maji,na Halmashauri ya Mufindi imetengewa kiasi cha Tsh.Bill 2.3,hivyo kwa kata mbili  zilizobakia,zenye uhaba wa maji kutokana na ukame atahakikisha ufumbuzi unafanyika kuondoa tatizo hilo.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Itandula Hezron Muyinga alisema kuwa kitendo cha mbunge huyo kuangazia sekta ya maji  ukizingatia maji ni muhimu sana katika Afya ya binadamu.
Muyinga alisema kulikuwa na kero kubwa  ya bupatikanaji wa maji katika shule za msingi,ambapo walimu walikuwa na wananchi walikuwa wanatembea umbali wa zaidi ya km 2 hadi 5 kutafuta maji ambayo hayakuwa safi na salama.Pia alisema wanamuunga mkono mh.mbunge kwa kuona umuhimu wa kuwapatia wananchi wa wilaya yake maji safi na salama
 ‘’’’Hapo awali maji yalikuwa yanauzwa ndoo moja kwa  kiasi cha Tsh. 500 ,hii ilikuwa ni kero kubwa kwa wananchi kukosa usingizi ,pamoja na walimu kupoteza muda wao mwingi kutafuta maji na kushindwa kutumia muda wao fundisha’’’’alisema Muyinga.




0 maoni:

Chapisha Maoni