Mkuu
wa mkoa wa Mwanza John Mongella, amewaapisha wakuu wapya wa Wilaya za
Mkoa wa Mwanza na kuwapa vitendea kazi ikiwapo katiba ya Jamhuri ya
muungano wa Tanzania na Ilani ya Chama Tawala Chama Cha Mapinduzi (CCM)
ya Mwaka 2015-2020, kwaajili ya kwenda kutimiza wajibu wao wa kikatiba
kwenye wilaya walizo pangiwa.
Akizungumza
baada yakuwaapisha, Mhe. Mongella, amewataka waende wakasimamie
shughuli za kuhimiza maendeleo, suala la ulinzi na usalama kwenye wilaya
zao, huku akitilia mkazo ukomeshwaji wa mauwaji ya watu wenye ulemavu
wa Ngozi albino pamoja na Vikongwe, amesema, ikiwa jamii ya watu hao
itapata madhara basi ni dhahiri Mkuu huyo wa Wilaya atakuwa ameshindwa
kusimamia majukumu yake.
Mkuu
huyo wa mkoa pia, amerudia kauli yake nakuwataka viongozi hao wapya
watambue wanajukumu zito lililoko mbele yao, ikiwa ni pamoja na
kukomesha Utumiaji wa dawa za kulevya.
Aidha
ameonya uchezaji wa Pool na unywaji wa Pombe wakati wa saa kazi, huku
akimsisitiza mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha ifikapo Agosti
mosi, suala la wafanya biashara wanaofanya biashara kwenye maeneo ambayo
hayaruhusiwi liwe limepatiwa ufumbuzi.
Mongella
amesema, katika mkoa wa Mwanza, Hotel na Clabu, yeyote ile, iwe ya
kawaida au ya Kitalii, ikibainika inafanya biashara ya Shisha, hawata
ivumilia na badala yake wataifutia Leseni ya biashara.
Walio
apa mbele ya Mkuu wa Mkoa, ambao waliteuliwa na Mhe. Rais Tarehe 26,
Juni, 2016 ni Emmanuel Enock Kipole, Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,
Estomin Francis Chang’a Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo
Mkuu wa Wilaya ya Magu, wengine ni Juma Samwel Sweda Mkuu wa Wilaya ya
Misungwi, Dkt. Leonard Moses Masale Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mary
Onesmo Tesha Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana na Mhandisi Mtemi Msafiri
Simioni Mkuu wa Wilaya ya Kwimba.
0 maoni:
Chapisha Maoni