Licha
ya Jumapili ya Juni, 3 vilabu vingi barani Ulaya kufanya usajili lakini
pia zilisambaa habari na picha zikimwonesha kiunga mshambuliaji wa
Manchester United, Juan Mata akiwa na jezi ya Everton ikiwa na maelezo
kuwa Mata amejiunga na klabu hiyo ya Everton.
Taarifa
za Mata kujiunga Everto zilisambaa zaidi katika makundi ya WhatsApp na
mashabiki wengi wa soka kuamini kuwa ni kweli mshambualiaji huyo rais wa
Hispania amejiunga a Everton ambayo imepata meneja mpya, Ronald Koeman.
Lakini
jambo hilo halina uhalisia na kimechofanyika ni kupotosha mashabiki wa
soka na uhalisia ni kwamba Everton inahitaji kumsajili Mata kwa kitita
cha Pauni Milioni 20 lakini bado hawajafikia makubaliano yoyote na
Manchester United.
Kama
Man United ikimuachia Mata basi moja kwa moja kocha mpya wa United,
Jose Mourinho anaweza kutajwa kuwa sababu kubwa ya kiungo huyo kuondoka
kwani hata wakati akiifundisha Chelsea alimuuza mchezaji huyo kwa sababu
kuwa haendani na kasi yake.
Pamoja
na Mourinho kuhusishwa na kumuondoa Mata mwingine anayetajwa ni kiungo
mshambualiaji wa Dortmund, Henrikh Mkhitaryan ambaye anacheza nafasi
moja na Mata na ikiwa tayari ameshadhibitishwa kujiunga Man United na
sasa akisubiri kufanyiwa vipimo hivyo kuchangia Mata kuwa rahisi
kuondoka Man United.
0 maoni:
Chapisha Maoni