Meneja
anayeshughulika na masuala ya Mazingira wa kampuni ya vinywaji ya
SABMiller kanda ya Afrika, Bw.Muzi Chonco, ambaye yuko nchini kwa ziara
ya kikazi mwishoni mwa wiki alifanya ziara katika Wizara ya Maji na
Umwagiliaji ambapo alikukutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Mhandisi Mbogo Futakamba.
Bw.Chonco
katika mazungumzo hayo aliweza kumweleza Katibu Mkuu miongozo na
mikakati mbalimbali ya kampuni hiyo kuhusiana na utunzaji wa
mazingira,matumizi sahihi ya maji ,utunzaji wa vya maji na miradi ambayo
kampuni inasaidia kuendesha.
Kampuni
ya SABMiller kwa hapa nchini inamiliki kampuni ya kutengeneza vinywaji
ya TBL Group ambayo inamiliki viwanda mbalimbali vya kutengeneza
vinywaji hapa nchini.
Katika
ziara hiyo ya kikazi Bw.Chonco aliongozana na Meneja wa kiwanda cha
kutengeneza bia cha TBL kilichopo Ilala jijini Dar es Salaam,Bw.Calvin
Martin na maofisa wengine wa kampuni ya TBL Group.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Mbogo Futakamba ( kulia)
akimsikiliza kwa makini Meneja mazingira wa SABMiller, Muzi Chonco,
wakati alipofanya ziara ya kikazi ofisini kwake Ubungo jijini Dar es
Salaam, (Kushoto) ni Meneja wa kiwanda cha bia cha TBL Group Ilala Dar
es Salaam Bw. Calvin Martin.
Katibu
Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Mbogo Futakamba (wa pili
kutokea kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Mazingira wa
SABMiller na Maofisa wa TBL Group walipomtembelea ofisini kwake mwishoni
mwa wiki iliyopita
0 maoni:
Chapisha Maoni