Chama
cha Soka barani Ulaya (UEFA) kimetangaza oodha ya wachezaji 10 ambao
watawania tuzo ya mchezaji bora wa mwaka barani Ulaya.
Katika
hali ambayo imewashangaza wengi, mshambuliaji wa Barcelona, Neymar
amekosekana katika oodha hiyo licha ya kuisaidia Barcelona kushinda
kombe la Liga kwa msimu wa 2015/2016 kwa kufunga goli 31 katika michezo
49.
Aidha
katika orodha hiyo, hakuna mchezaji hata mmoja wa ambaye anacheza Ligi
Kuu ya Uingereza hali ambayo inafanya kuwepo na mtizamo tofauti kuhusu
ubora wa ligi hiyo.
Wachezaji
ambao wametajwa ni Gareth Bale, Gianluigi Buffon, Antoine Griezmann,
Toni Kroos, Thomas Muller, Manuel Neuer, Luis Suarez, Pepe, Cristiano
Ronaldo na Lionel Messi.
0 maoni:
Chapisha Maoni