Posted by Esta Malibiche July 7/6/2016
in SIASA
|
![]() | ||||
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi ccm Iringa mjini Abeid Kiponza akizungumza na wandishi wa habari |
Chama cha Mapinduzi ccm Iringa mjini kimejipanga kuhakikisha kinalinda
mkutano mkuu wa ccm unaotarajiwa kufanyika tarehe 23/7/2016 mkoani Dodoma,kuwa
unafanyika kwa Amani na utulivu kama
ilivyopangwa.
Akizungumza na wandishi wa
Habari katika ofisi za ccm wilaya ya Iringa
,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa Mjini Abed Kiponza alisema
nimesikitishwa sana na kitendo cha
baraza la vijana chadema Bavicha kutoa tamko la kutaka kuzuwia mkutano mkuu wa
ccm usifanyike.
‘’’’’Natamka kwa niaba ya wanaccm
Iringa Mjini,na tutakabilana na yeyote atakaeleta vurugu ama kuonyesha dalili
za uvunjifu wa Amani.Tumejipanga na tuko tayari kupambana na wale wote
wataoleta fujo za makusudi wakati mkutano mkuu ukiendelea hatutamvumilia. ‘’’’’alisema
Kiponza.
Kiponza alisema kuwa mkoa wa Iringa
inaunga mkono juhudi zinazifanywa na Dr. john Magufuli kwa kuiletea heshima ccm
na Tanzania kwa ujumla.
Alisema wanaccm Iringa wanamuunga mkono
kwa asilimia mia moja na hawatasita kumpigia kura za ndiyo mwenyekiti mpya wa
chama hicho Taifa Dk John Magufuli ili aendelee kutekeleza yote yaliyoandikwa
katika Ilani ya chama hicho kwa lengo la kukijenga chama na serikali kwa ujumla
Kiponza alisema kuwa Dk Magufuli
ambaye ni rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM kwa muda
alioingia madarakani amefanya mambo mengi yanayoyafanya watanzania na hata watu
walio nje ya nchi kukubaliana na utendaji wake.
“Tunampongeza rais wetu mchapazi Dk
John Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kwa ajili ya maendeleo ya taifa
letu,kazi anayoifanya siyo tu inamletea heshima yeye bali inaliletea heshima
Taifa letu linaloaminiwa na kupendwa duniani”’’’alisema Kiponza
“Tunamtaka Magufuli achukue chama na
kuja kutekeleza yote anayoyafanya kwa lengo la kuimarisha chama chetu,pia
tunampongeza mwenyekiti wetu anayetarajia kukabidhi chama Jakaya Kikwete kwa
kuwa ametekeleza wajibu wake kwa kipindi cha miaka kumi na kuiacha nchi katika
hali ya amani”’’’’alisema.
Aidha Kiponza aliviomba vyombo vya
ulinzi na usalama kuwa makini na kundi hilo ambalo linahatarisha Amani ya Nchi kuwachukulia
hatua sitahiki ili taifa liendelee kubaki katika hali nya amani na utulivu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa
Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UV CCM)Iringa Mjini Kaunda Mwaipyana
alisema jumuiya ya vijana wilayani humo imejipanga kulinda mkutano huo na licha
ya vitisho kutoka kwa vijana wa Chadema wanaondai watazuia mkutano huo.
Kaunda alisema Uvccm Iringa Mjini wamepokea
kwa masikitiko makubwa tamko la baraza
la vijana la Chadema lililotangaza kuzuia mkutano huo usifanyike na kuongeza kuwa
Uvccm wilayani humo wamejipanga kwenda Dodoma
kuhakikisha ulinzi unaimarika na hawatamvumilia mtu yeyote atakaeleta vurugu za makusudi katika eneo linalofanyika mkutano
“Sisi vijana tumejipanga kuulinda
mkutano huo tunaomba viongozi wetu wawe na amani kwani jukumu la ulinzi wa
chama na mali za chama ni jukumu la UV CCM|”.alisema Mwaipyana.
Joseph Mgongolwa ni mlinzi wa chama wilaya ya Iringa nae aliwashauri vijana
wa Bavicha waliojipanga kwenda Dodoma kuzuia
mkutano huo kuacha mara moja kwa kuwa kitendo hicho kinaweza kuwasababishia
matatizo makubwa
Nimemuelewa sana Mzee KIPONZA
JibuFuta