Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla jioni ya jana Julai 8.2016, amezindua rasmi Shirika
la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF) inayojishughulisha na masuala ya Afya
Nchini Tanzania sambamba na kuzindua Programu maalum ya “NURU YA AFYA”.
Tukio
hilo ambalo Dk. Kigwangalla alikuwa mgeni rasmi, pia lilienda sambamba
na uzinduzi wa mpango maalum wa kutoa elimu na tiba ujulinakanao kama
“NURU YA AFYA” ambapo mpango huo unatarajia kuanza kwa Wilaya ya
Bagamoyo kwa kuweka kambi maalum na kutoa huduma mbalimbali za kiafya
pamoja na elimu huku lengo likiwa ni kuwafikia watu zaidi ya 500 kwa
kila baada ya miezi mitatu.
Awali
akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Dk. Kigwangalla alipongeza juhudi
za taasisi binafsi kwa namna zinavyojitolea kuisaidia Serikali katika
mapambano hivyo wataendelea kuziunga mkono kwa hali na mali.
“Naomba
nichukue fursa hii kuwashukuru kwa kuanzisha kitu kama hiki kwani ni
jambo jema na munaisaidia Serikali katika kufikia malengo yake. Naamini
shirika kama hili TAHMEF ambapo wengi wenu ni vijana na wasomi hasa
katika kada ya Afya ni chachu kubwa sana ya kufikia malengo katika sekta
ya Afya ya Nchini.
Watu
wengi wanaamini Serikali pekee yake ndio wenye jukumu la kutatua
matatizo katika Sekta ya Afya. Bali suala hili ni letu sote hivyo kwa
uwepo wenu ni fursa ya kipekee kwa nanyi kusaidiana na Serikali katika
kufikia malengo yake,” alieleza Dk. Kigwangalla katika uzinduzi huo.
Hata
hivyo Dk. Kigwangalla alieleza kuwa, Vijana hao wameonyesha uthubutu
ambapo amewatakia kila la kheri katika shughuli zao hizo.
Aidha,
Dk. Kigwangalla pia aliweza kuendesha harambee ndogo ya kusaidia
taasisi hiyo na watu mbalimbali waliweza kujumuika kuichangia.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Shirika la Afya na Elimu ya
Tiba (TAHMEF), Bi.Juliana Busasi alieleza kuwa wakiwa kama vijana
wamekuwa na malengo makubwa ya kusaidiana na Serikali hasa katika Afya
hivyo amemuhakikishia Naibu Waziri wa Afya kuwa, shirika lao itafanya
kazi bega kwa bega na Wizara yake pamoja na wadau wengine katika kufikia
malengo yaliyopo hapa nchini.
Nae
Mkurugenzi wa Miradi wa shirika hilo, Hansi Olomi amebainisha kuwa, ili
kufikia malengo, TAHMEF inatarajia kuendesha miradi mbalimbali ambapo
wataanza na mradi wa “NURU YA AFYA” ambao unatarajia kuanza Bagamoyo
Mkoani Pwani kuanzia Mwezi Oktoba Mwaka huu.
Mradi
huo wa Nuru Yetu, ni miongoni mwa miradi ya shirika hilo ambapo
watakuwa wakitoa huduma ya Afya na Elimu kwa watu mbalimbali hapa nchini
ambapo kwa kuanzia wataanza na Wilaya ya Bagamoyo.
Shirika
hilo ya TAHMEF inaundwa na vijana wanaosomea kada ya Udaktari katika
vyuo vya tiba hapa nchini ikiwemo wale wa Hubert Kairuki, Muhimbili pia
wapo kutoka Chuo kikuu cha Mlimani (UDSM) na wengineo.
Mwenyekiti wa baraza la chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Prof. Esther Mwaikambo,
(Pichani Juu) akisalimiana na Dk. Kigwangalla wakati alipowasilia
katika ukumbi wa mikutano uliopo katika hoteli ya Seashells Milllennium
Hotell-LAPF Tower Jijini Dar es Salaam
Edmond Issae wa taasisi ya TAHMEF akitoa neno fupi la ufunguzi wa tuko hilo, Kulia ni Kijanana Willson ambaye alikuwa MC.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla akifuatilia uzinduzi huo wa taasisi ya TAHMEF
Mwenyekiti na Mwanzilishi wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), Bi.Juliana Busasi akitoa maelezo mafupi juu ya shirika hilo kwa wageni waalikwa (hawapo pichani)
Kiongozi wa
Miradi ya shirika hilo la TAHMEF, Hans Olomi akielezea namna
walivyojipanga kuendesha miradi yao kwa njia ya kitaalam ikiwemo kutumia
ujuzi wao katikak Sekta ya Afya
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akizindua rasmi shirika la TAHMEF.
Meza kuu
Wageni waalikwa wakiwa meza kuuNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa hutuba fupi ya uzinduzi huo.
Dk.
Kigwangalla akitoa maelezo namna Serikali inavyojitahidi kusaidia Sekta
ta Afya hapa nchini huku wakiimiza wadau kuwa mstari wa mbele
kusaidiana nayo.
Baadhi ya wanachama wa Shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF) pamoja na wageni wengine waalikwa.
Mchora
vibonzo maarufu na Mhariri wa katuni wa ITV, Bwana Nathan Mpangala
akifuatilia kwa umakini uzinduzi huo. Nathan ni miongoni mwa wadau wa
shirika la TAHMEF.
Wageni waalikwa.
Mwenyekiti wa baraza la chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Prof. Esther
Mwaikambo (kushoto) akiwa pamoja na Bi. Kokushubira Kairuki ambaye ni
Mwenyekiti wa Hubert Kairuki University wakifuatilia tukio hilo.
Miongoni mwa vijana walioanzisha shirika hilo ni wanafunzi wa udaktari
katika chuo hicho cha Kairuki
Nathan Mpangala akitoa ahadi yake katika harambee fupi ya kuchangia mradi wa NURU YA AFYA wa shirika la TAHMEF.
Moja ya picha iliyokuwa ikinadiwa katika harambee hiyo.
Nathan akisalimiana na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla
Dk. Kigwangalla akieleza jambo kwa Pastor Maestro ambaye pia ni Naibu Mkurugenzi wa CDC
Bi. Kokushubira Kairuki ambaye ni Mwenyekiti wa Hubert Kairuki University akitoa ahadi ya kuchangia shirika la TAHMEF
Wageni waalikwa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano wakiahidi kuchangia shirika la TAHMEF
Wageni waalikwa kutoka Mamlaka ya Mawasiliano wakiahidi kuchangia shirika la TAHMEF
Dk.
Kigwangalla akipokea picha ya mchoro ambayo ilitolewa kwake baada ya
kuinunua kwa Sh. Milioni moja na nusu katika Harambee ya kuchangia shirika la TAHMEF
Pastor Maestro akipokea picha ambayo aliichangia katika Harambee hiyo
Dk.
Kigwangalla akpokea keki maalum ambayo alikabidhiwa kama zawadi kwa
mchango wake wa kuthamini shughuli za taasisi binafsi katika mchango wa
kufikia malengo kwenye sekta ya Afya.
Dk.
Kigwangalla akpokea keki maalum ambayo alikabidhiwa kama zawadi kwa
mchango wake wa kuthamini shughuli za taasisi binafsi katika mchango wa
kufikia malengo kwenye sekta ya Afya.
Mwenyekiti na Mwanzilishi wa shirika laTAHMEF, Bi.Juliana Busasi akimshukuru mgeni rasmi kwa kuzindua rasmi taasisi hiyo.
Dk. Kigwangalla akikata keki maalum
Dk. Kigwangalla akimlisha keki Bi. Kokushubira Kairuki ambaye ni Mwenyekiti wa Hubert Kairuki University
Dk. Kigwangalla akimlisha keki Mwenyekiti wa Baraza la chuo Kikuu cha Tumaini Makumira, Prof. Esther Mwaikambo.
Dk. Kigwangalla akimlisha keki Pastor Maestro.
Dk. Kigwangalla akimlisha keki Mwanzilishi na Mwenyekiti wa shirika la TAHMEF, Bi. Juliana Busasi
Pia kulikuwa na burudani kidogo….
Wageni waaliwa wakifuatilia tukio hilo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla akipata picha na wageni wengine waalikwa pamoja na
viongozi wa shirika la TAHMEF
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akipata picha na baadhi ya viongozi wa TAHMEF.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akipata picha na baadhi ya vijana wanaosomea kada
Udaktari ambao walialikwa katika tukio hilo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akipata picha na baadhi ya vijana wanaosomea kada
udaktari ambao walialikwa katika tukio hilo
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla akipata picha ya ukumbusho na wanafunzi wanaosomea
Udaktari hapa Nchini.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla akipata picha ya ukumbusho na wanafunzi wanaosomea
Udaktari hapa Nchini
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akipata picha ya ukumbusho na wanafunzi wanaosomea Udaktari
hapa Nchini
Profesa Mwaikambo akipata picha ya pamoja na Juliana.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla akipata ‘selfie’ na picha ya ukumbusho na wanafunzi
wanaosomea Udaktari hapa Nchini ambao wameamua kuanzisha taasisi ya
kusaidia jamii katika sekta ya Afya ijulikanayo kama TAHMEF. (Picha zote
na Andrew Chale,
0 maoni:
Chapisha Maoni