Mtoto
Happiness John Mkazi wa Seliani Arusha aliyefanyiwa upasuaji kwenye
moyo na kupandikiziwa kifaa cha kusaidia kudhibiti mapigo ya moyo
(pacemaker), ameanza mazoezi.
Daktari
Bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto, Sulender Kuboja aliyeshiriki
upasuaji huyo alisema jana kuwa hali ya mtoto huyo inaendelea vizuri na
wameanza kumfanyia mazoezi mepesi.
Dk
Kuboja alisema kwa kawaida mgonjwa yeyote aliyefanyiwa upasuaji
anapaswa kufanyiwa mazoezi mepesi na kwamba kwa mtoto, mazoezi
anayofanyiwa ni ya kukaa, kusimama na kutembea kidogo.
“Hali
yake inaonekana kuendelea vizuri sana... nimetoka kumfanyia vipimo muda
mfupi uliopita kifaa kile kinafanya kazi vizuri na maendeleo yake
yanaridhisha sana,” alisema Dk Kuboja.
Alisema mtoto huyo anaweza kuongea na hata kula chaku- la, hali aliyosema inaonyesha nafuu nzuri kwake.
Mama
mzazi wa mtoto huyo, Elitruda Malley alisema anaridhishwa na maendeleo
ya afya ya mwanaye kwa kuwa tangu afanyiwe upasuaji huo juzi, hali yake
imeonekana kuimarika kwa haraka.
Mama
huyo alisema tangu awekewe kifaa hicho, mwanaye amekuwa mchangamfu,
hali aliyosema inamtia moyo na kumpa matumaini makubwa.
“Ingawa
yupo kwenye oxygen, lakini namshukuru Mungu kwani anaonekana anapata
nafuu nzuri, anatabasamu na kuongea vizuri kabisa na ana furaha sana,
shauku yake ni apone ili aende shule kama watoto wengine,” alisema Malley.
Aliongeza kuwa mtoto huyo amekuwa akila vizuri na kumpa moyo kwani mwili wake unaonekana kuwa na nguvu na afya nzuri.
“Madaktari
wapo karibu wakifuatilia afya ya mtoto kwa ukaribu, wanampa chakula,
wanamfanyia mazoezi ya kukaa na kushuka chini, anaonekana kuwa na nguvu
na mwenye maendeleo mazuri. "
Alisema
jambo linalompa faraja ni kuona jinsi madaktari wote wanaomuhudumia
mtoto huyo wanavyofanya kazi hiyo kwa upendo na bidii.
Juzi,
kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI) ilifanikiwa kumpandikiza mtoto huyo mwenye umri wa
miaka mitano kifaa cha kusaidia kudhibiti mapigo ya moyo (pacemaker)
kinachoendeshwa kwa betri.
Hayo
ni mafanikio ya pili kwa taasisi hiyo ya kisasa ukanda wa Afrika
Mashariki na Kati baada ya Mei 24 na 25, mwaka huu kufanikisha
operesheni kwa wagonjwa 18 bila kuusimamisha moyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni