Licha
ya kutokushinda taji lolote kwa msimu wa 2015/2016 lakini bado hilo
halijawa kigezo cha wamilikiwa klabu ya Liverpool kukataa kuendelea
kufanya kazi na kocha wa klabu hiyo, Jurgen Klopp.
Liverpool
imetoa taarifa kuwa imemuongezea mkataba mrefu zaidi wa miaka sita
kocha wake, Klopp ili aendelee kuinoa klabu hiyo mpaka mwaka 2022
maamuzi ambayo yamekuja baada ya kuibadilisha Liverpool kwa kiasi fulani
japo haikwataa taji lolote lakini ilifanikiwa kufika hatua ya fainali
ya Uefa Europa.
Pamoja
na Klopp kuongezewa mkataba, pia makocha wasaidizi wa mjerumani huyo,
Zeljko Buvac na Peter Krawietz nao wameongezea mkataba sawa na mkuu wao
wa kazi, Klopp.
Taarifa
ya Liverpool inaeleza kuwa uamuzi wa kumuongezea Klopp mkataba ulikuja
siku ya Jumatano ambapo wamiliki wa klabu, Fenway Sports Group (FSG)
walitaka kuendelea kufanya kazi na Klopp kwa miaka mingi na ndipo
walipofanya nae mazungumzo na baada ya kukubaliana amesaini mkataba
mwingine.
Akizungumza
na mtandao wa Liverpool, Klopp amesema “Ni ngumu kuelezea kwa maneno
jinsi ambavyo ninajisikia mimi, Zeljko na Peter kwa jinsi
tumevyokubalika kwa wamiliki wa timu na kwa klabu kwa ujumla”






0 maoni:
Chapisha Maoni