Baada ya Uingereza kutolewa katika michuano ya Euro na kumfukuza aliyekuwa kocha wake, Roy Hodgson na kuanza kutajwa baadhi ya makocha wanaoweza kukabidhiwa mikoba ya kocha Hodgson, mmoja wapo ni kocha wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye na yeye ameonyesha nia ya kuifundisha timu ya taifa ya Uingereza.
Mbali na maelezo ambayo ameyatoa kocha huyo kuwa Uingereza inafuatia kuwa nyumbani kwake baada ya Ufaransa lakini pia kumekuwepo na taarifa za chini ya kapeti kuwa kocha huyo hana uhakika kama ataongezewa mkataba na Arsenal pindi utakapomalizika mwakani 2017.
Akizungumza na kituo cha michezo cha beIN Sports, Wenger alisema “Nikitakiwa kuiongoza Uingereza? Kwanini nikatae? siwezi kulipinga hilo, lakini nina furaha kuongoza klabu,
“Uingereza ni nchi yangu ya pili, nilishangazwa na Uingereza kutolewa na Iceland, sikuamini hilo,” alisema Mourinho na kuongeza.
“Ukiangalia mchezo wao unaweza kupata picha jinsi ilivyo, baada ya dakika ya 60 kama kuna vitu vibaya vimewapata, walikuwa wamechanganywa na mchezo au wamechoka? Sijui lakini Uingereza wanatakiwa kutafuta jawabu kwa kilichowatokea dhidi ya Iceland”