Ijumaa, 6 Mei 2016

Ujumbe wa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova kwa Siku ya Dunia ya Urithi wa Kiafrika, 5 Mei 2016 0



Siku ya Dunia ya Urithi wa Kiafrika ni siku muhimu sana.
Ni fursa ya kusherehekea utajiri wenye thamani kuu wa urithi wa utamaduni na asili ya Afrika. Huu ni wakati wa dunia kusimama na serikali, wanajamii na jumuia mbalimbali ili kusaidia moja ya rasilimali yenye thamani kuu zaidi katika bara hili. Urithi na kiutamaduni na asili wa Afrika ni nguvu kubwa amani na pia ni kichocheo cha maendeleo na uvumbuzi.
Msukumo wa siku hii ya kimataifa, kama ilivyotangazwa na nchi wanachama wa UNESCO mwezi Novemba 2015, ni kuongeza uelewa wa kimataifa wa urithi wa Afrika na kuhamasisha ushirikiano mkubwa katika kuulinda urithi huu. Hii inajumuisha kila mtendaji, kuanzia kwa watoto wa shule, vijana wa kike na wa kiume  na wadau wote, ikiwa ni pamoja na Mfuko wa Kimataifa wa Urithi wa Afrika , ambao mwaka huu  unaadhimisha mwaka wake wa kumi.
Katika muongo uliopita, tumefanya maendeleo makubwa ya kuongeza idadi ya maeneo ya Afrika kwenye orodha ya urithi wa Dunia, hii ikienda pamoja na kuboresha uhifadhi na usimamizi, kupanua ushiriki wa jamii na kuongeza faida kwa jamii. Hata hivyo, kati ya maeneo 129 ya kiutamaduni na asili katika bara la Afrika yaliyoorodheshwa katika ya orodha ya urithi wa dunia, kuna maenoo 17 yaliyopo pia kwenye orodha ya maeneo ya urithi wa dunia yaliyomo hatarini. Hatari zinazotishia maeneo hayo ni nyingi, ikiwa ni pamoja na vita, ugaidi, ujangili,ongezeko la joto duniani, upanuzi wa miji, na utafutaji wa mafuta na madini, yote haya yanayojitokeza wakati kukiwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi na kijamii.
Kulinda na kukuza urithi wa kiutamaduni na asili ya Afrika ni kitu kilicho katika kiini cha kazi ya UNESCO ya kuendeleza heshima na maelewano, na kulinda vyanzo vya uasili na ubunifu. Hii pia ni muhimu katika kuendeleza Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu – kulinda urithi husaidia kutengeneza nafasi za kazi, kukuza usawa wa kijinsia, na kuondoa umaskini. Hakuna haja ya kuchagua kati ya urithi na ukuaji, kati ya mandhari nzuri na maisha ya heshima – tukiwa na ujuzi sahihi na uwezo ulio bora tunaweza kutumia urithi wa kiutamaduni na asili kutengeneza ya ajira nzuri, na hivyo hali njema ya utu na heshima. Kwa kuhifadhi maliasili, mito na mbuga, tunaweza kuwa na vyanzo vya ajabu mno vya nishati mbadala kwa wote. Hakika, hili ni jambo la jema kulifanya na uamuzi ulio makini. Huu ni ujumbe wa UNESCO leo.
Hii ni muhimu kwa Afrika – kwa wanawake na wanaume duniani kote, na hasa kwa vijana

0 maoni:

Chapisha Maoni