TIB
Corporate Bank imesema imekusudia kuwawezesha kifedha wakandarasi wa
ndani ili waweze kutekeleza vema majukumu yao ya kikandarasi.
Akizungumza
wakati wa mkutano wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi nchini (CRB)
uliofanyika jijini Mwanza, Mkuu wa Kitengo cha Mauzo ya Mikopo wa Benki
ya TIB, Theresia Soka amesema benki yake imekuja na suluhisho la kutatua
changamoto za wakandarasi wazawa.
TIB
Corporate Bank imemua kurahisisha taratibu zake za kutoa mikopo kwa
wakandarasi wa ndani kwa kuwataka kuwasilisha vielelezo tu
vinavyomtambulisha kuwa amesajiliwa kisheria ili aweze kupata mkopo.
‘Tumeamua
kurahisisha utaratibu wetu wa utoaji mikopo ili kuwawezesha wakandarasi
na hivyo kuchangia ukuaji wa maendeleo nchini katika sekta hii muhimu
ya ujenzi’ alisema Bi Soka.
Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TIB Corporate, Bahati Minja
(aliyesimama) akitoa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na TIB
Corporate Bank.
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa TIB Corporate Bahati Minja,
alisema benki hiyo inayomilikiwa na Serikali, imeboresha huduma zake za
kibenki ili kuwawezesha wakandarasi wazawa.
‘Lengo
kubwa la Benki ya TIB Corporate ni kuhakikisha wakandarasi wanawezeshwa
kifedha ili wawe na vitendeakazi vya ujezi’ alisema Bi Soka.
Hata
hivyo wakandarasi waliohudhuria mkutano huo ambao miongoni mwao
wamefadhiliwa na benki hiyo, waliupongeza uongozi wa Benki ya TIB
Corporate kwa kuamua kuwawezesha kwa mikopo ya kikandarasi.
Wakandarasi
hao walisema uwezeshwaji huo wa mikopo nafuu inayotolewa na benki hiyo,
itawasaidia kuendesha kampuni zao za ujenzi kwa ufanisi zaidi.
Mkutano
huo wawakandarasi wenye kauli mbiu ya ‘Kuwajengea Uwezo Wakandarasi wa
Ndani kwa ajili ya Uchumi Endelevu’, utafuatiwa na mkutano mwingine
utakaofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Daimond Jubilee
kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa tano.
TIB
Corporate Bank imefanya mabadiliko ya kitaasisi ili kuweza kuwa kituo
cha huduma zote za kibenki kwa kushughulikia mahitaji ya wawekezaji wa
ndani kwa lengo la kusukuma maendeleo ya uchumi wa Taifa
0 maoni:
Chapisha Maoni