Picha za gari lililokuwa na ujumbe wa kukasirisha uliochorowa katika gari hilo zimesambazwa mara elfu katika mtandao wa Twitter.
Gari hilo
jeupe aina ya Range Rover Revere lenye bei ya pauni 75,000 lilionekana
limeegeshwa karibu na Harrods magharibi mwa London na kuchorwa ujumbe wa
kukasirisha kwa kile kilichoonekana kuwa mpenzi aliyedanganywa.
Gari hilo
liliandikwa 'cheater' { mwongo} katika pande zote mbili za gari huku
maneno ''Natamani angekuwa na thamani'' yakiandikwa katika madirisha ya
gari hilo.
Klo ambaye alipiga picha za gari hilo alisema kuwa alimuona mwanamke mmoja akilichora gari hilo,alikuwa kama aliye na wazimu.
'Hakuna
mtu aliyejaribu kumzuia.Baadaye aliondoka.Maneno ''Its Over'' pia
yaliandikwa kwenye gari hilo ikielezea kuisha kwa uhusiano wowote''
0 maoni:
Chapisha Maoni