Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa
mafunzo ya matumizi ya huduma za mawasiliano kwa watumishi wa Wizara ya
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kupata muongozo utakaowasaidia
kuepuka matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.
Akifungua mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bi. Nuru Mllao amewataka watumishi wa wizara hiyo kuzingatia mafunzo hayo ili kuepuka matatizo ya mitandao ya kijamii wakati wakuteleza majukumu yao.

“Tumegundua kwamba watumishi wanahitaji
muongozo juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii, hivyo tunashkuru
sana uongozi wa TCRA kukubali kutoa mafunzo kwa watumishi wetu”alisema
Bi.Nuru.
Aidha Bi Nuru ametoa rai kwa TCRA kutoa mafunzo hayo kwa watumishi wa wizara nyingine kwa kuwa watumishi wote wanatakiwa kupata miongozo juu ya matumizi sahihi na usalama wa huduma hizo.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Mhandisi James Kilaba, alisema kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii yameongezeka hivyo kuchangia kuongezeka kwa changamoto za matumizi mabaya ya mitandao hiyo.

Kwa upande wa huduma za mawasiliano ya simu,
Mhandisi Kilaba alisema kuwa mawasiliano ya simu yanakua kwa kasi nchini
hali ambayo inaongeza matumizi mabaya ya mawasiliano ya simu.
“Idadi ya laini za simu kwa miaka 12 iliyopita
ilikuwa ni milioni 2.3 lakini hadi kufikia mwezi Machi mwaka huu idadi
ya laini ni takribani milioni 40, wananchi ni wengi wanaotumia huduma za
mitandao na wengi wao wanaitumia vibaya”alisema Muhandisi Kilaba.
Mhandisi Kilaba alielezea kuwa mafunzo hayo
yataegemea kwenye nyanja za kukua kwa sekta ya mawasiliano na changamoto
zake pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia katika matumizi ya mitandao
ya kijamii.
Alisisitiza kuwa kupitia mafunzo hayo watumishi wataweza kujua matumizi sahihi ya mitandao hasa katika shughuli zao za kiofisi.
Katika kuzingatia usalama wa mawasiliano yao,
TCRA imewashauri watumishi pamoja na wananchi kwa ujumla kutotumia
nywila (password) moja kujiunga kwenye mtandao zaidi ya mmoja.
Aliwataka kutoweka nywila ambazo zinahusisha
mambo binafsi ambayo yanajulikana kwa watu wengi ili kuzuia mtu mwingine
asipate urahisi wa kubuni kuingia katika mtandao wa mtu mwingine.
0 maoni:
Chapisha Maoni