Afisa
maendeleo ya vijana mkoa wa Iringa Atilio mganwa amewataka vijana kote nchini,
kujiunga katika vikundi ili waweze kunufaika na asilimia inayotolewa na
serikali kwa kila Halmshauri.
Akizungumza
na mtandao wa kali ya habari leo ofisini kwake alisema ili kupunguza wimbi kubwa
la vijana wasio na ajira nchini vijana wanatakiwa kubadilika kwa kubadili mtazamo
wa kususubiri kuajiliwa na hatimae kujiajiri wenyewe kwa kutumia fursa
zinazotolewa na seriakali.
Atilio
alisema serikali ilishatoa maelekezo kwa kila Halmashauri nchini kutenga
asilimia kumi,ambapo 5% ni kwa ajili ya vijana na 5% kwa ajili ya wananwake kwa
lengo la kuwainua kiuchumi.
Alisema
vijana wanaonufaika na fedha hizo ni
wale waliojiunga waliojiunga katika vikundi,ambao wanapewa mikopo ya fedha na
hatimae kujiajili wenyewe kwa kufanya
shughuli mbalimbali.
Alisema
vijana wanapaswa kuendana na usasa kwa kujiajili wenyewe hasa katika kuchanganua
shughuli za kufanya hasa katika kilimo ambacho
kinaweza kubadili maisha yao na kuachana na tabia ya utegemezi pamoja na kuaka vijiweni
kupisga soga zisizo na msingi.
Ili tuweze
kuendanan na kasi ya Rais Dkt Magufuli vijana tunatakiwa tufanye kazi kwa bidii
zaidi kila mmoja kwa nafasi yake mahali
alipo ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa
na serikali ya awamu ya tano.
Atilio
alisema pamoja na hayo vijana wanakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa maeneo ya kuendeshea
shughuli zao kama kilimo na biashara kutokana na Halmashauri pamopja na
serikali za vijiji kushindwa kutenga eneo maalumu kwa ajili ya vijana na
hatimae kukodi na kushindwa kumudu gharama hizo
Vijana
wanashindwa kuendesha shughuli zao kwasababu ya kutotengewa nmaeneo yao
maalumu,Hali hii inasababisha kushindwa kufanya kazi zao hasa katika kilimo na
biashara.Asilimia kubwa ya vijana nchini wako vijjijini na wanategemea kilimo
na biashara ndogondogo,hivyo serikali kwa kupitia Halmashauri zetu inatakiwa
kuona umuhimu wa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya vijana ili waweze
kuendesha shughuli zao ya vijanan walio’’’’’’’ alisema
Kutokana na
hali hiyo tumepanga mikakati kwa mkoa mzima kwa pamoja tumeshawishi kila
Halmashauri ifungue SACOS ya vijana ili
na tayari zimefunguliwa katika wilya ya Mufindi,Kilolo,Iring mjini,Iringa
vijijini na katika Halmashauri ya Mji wa Mafinga Mchakato wa ufunguzi unaendelea’’’’’alisema
Alisema
sacos hizo zitasaidia waliopo katika
vikundi kjipatia fedha na kujiajili wenyewe,hali itakayosaidia kujiajili na
kuachanan na utegemezi na kusubiri kuajiliwa na serikali pekee.
Kama
unavyojua vijana waliowengi wanafikiri serikali pekee ndiyo inayoweza waletea
maendeleo yao binafsi baada ya kuajiliwa wakati kuna fursa nyingi hasa katika
kilimo,kwani vijana wengi wanadhani swala la kilimo ni la wazee tu.wakati ni
sasa ambapo watanzania tunatakiwa kuamka’’’’’alisema
Aidha
aliwaasa vijana kujiepusha na maradhi ya kuambukizwa ambayo yanaweza waletea
madhara ya kiafya na kushindwa kuendeleza shughuli zao za kimaendeleo kwa
manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
0 maoni:
Chapisha Maoni