Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha
Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza katika
Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza
Dkt. Asha-Rose Migiro mara baada ya kumuapisha kuwa Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza katika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini
Uingereza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi John Kijazi katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani
Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza
pamoja na Profesa Cleophas Migiro mme wa Dkt. Asha-Rose mara baada ya
tukio la uapisho katika Ikulu ndogo ya Chwamwino mkoani Dodoma.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Dkt. Asha-Rose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza huku
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje
Balozi Augustine Mahiga wakisikiliza.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia
jambo na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mara baada ya kutoka kwenye
tukio la kumuapisha Dkt. Asha-Rose Migiro kuwa Balozi mpya nchini
Uingereza . PICHA NA IKULU
…………………………………………………………………………………………………………………………
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuapisha Dkt. Asha-Rose Mtengeti
Migiro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Hafla ya kuapishwa kwa Dkt.
Asha-Rose Mtengeti Migiro imefanyika leo tarehe 05 Mei, 2016 katika
Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Peter Kallaghe ambaye amerudishwa nyumbani.
Akizungumza baada ya kuapishwa,
Dkt. Migiro ameahidi utumishi uliotukuka na kwamba atahakikisha uhusiano
na ushirikiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na
Uingereza unaimarishwa zaidi, hususani katika kuvutia uwekezaji,
biashara na utalii baina ya nchi hizi mbili.
Dkt. Migiro pia ametoa wito kwa
watanzania waliopo hapa nchini na waishio Uingereza kuitumia ofisi hiyo
ya ubalozi ipasavyo, ili waweze kunufaika na fursa mbalimbali hasa za
kiuchumi.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
05 Mei, 2016
0 maoni:
Chapisha Maoni