Wawakilishi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma nchini wakifuatilia mada
Mkurugenzi
Msaidizi Bi. Veila Shoo akiwasilisha matokeo kuhusu Ufuatiliaji wa
Mifumo na Viwango vya utendaji kazi kwa Taasisi za Umma
nchini.Wanaomsikiliza ni sehemu ya wawakilishi kutoka katika Taasisi za
Umma.
……………………………………………………………………………………………….
Taasisi za Umma zimehimizwa kutumia ipasavyo mifumo ya utendaji kazi iliyowekwa ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mkurugenzi Msaidizi ,Ofisi ya
Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bi. Veila Shoo alisema hayo wakati
akitoa takwimu za matumizi ya mifumo hiyo katika kikao kazi
kilichohusisha wawakilishi kutoka katika Wizara, Idara Zinazojitegemea
na Wakala za Serikali na kufanyika katika ukumbi wa Ofisi ya
Rais-Utumishi.
Bi. Veila alieleza kuwa
ufuatiliaji wa mifumo umefanyika katika Idara Zinazojitegemea 16 ambapo
imebainika baadhi ya mifumo inatukima ipasavyo wakati mingine bado.
Awali, akifungua kikao kazi hicho
Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick Kiliba
alisema kuwa zoezi la kufanya ufuatiliaji wa mifumo ni endelevu na
watendaji wanatakiwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo kwa
kutumia mifumo hiyo.
Alisema lengo la tathmini hiyo ni
kupata takwimu za utekelezaji wa mifumo na viwango vya utendaji kazi,
kutambua mifumo yenye changamoto za utekelezaji, kutoa hamasa ili
kuboresha utoaji huduma na kutoa mrejesho kwa taasisi jinsi ya
kuimarisha mifumo.
Mifumo iliyofanyiwa tathmini ni
pamoja na:- Mpango mkakati Mkataba wa Huduma kwa Mteja; Mfumo wa wazi wa
Tathmini ya Utendaji kazi; Uboreshaji wa michakato ya Utoaji huduma;
Tathmini ya Utoaji huduma wa Taasisi; Tathmini ya ndani ya Taasisi;
Ushirikiano wa Taasisi ya Umma na Asasi za Kiraia(AZAKI); Waraka Namba 1
wa mwaka 2012 kuhusu Ununuzi wa Samani za Ofisi; na Usimamizi wa Fomu
za Serikali.
0 maoni:
Chapisha Maoni