BABA
Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati)
akiwa na Katibu Mkuu wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) Michael
Kagondela kulia na Mhasibu wa mtandao huo, Asha Salvador baada ya
kumkabidhi kadi ya uanachama na katiba baada ya kikao cha kuthibitisha
mwanae kukubali kupewa ekari tano za kujenga kituo cha wanamichezo,
Mkuranga
BABA
Mzazi wa Mchezaji bora wa Soka bara la Afrika, Ali Samatta (katikati)
akijaza fomu za kukubali masharti ya kujiunga na Mtandao wa Wasanii
Tanzania (SHIWATA) mbele ya Mhasibu wa mtandao huo Asha Salvador.
………………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu
MTANDAO wa Wasanii Tanzania
(SHIWATA) umeandaa sherehe za kumkabidhi eneo la kujenga kituo cha
michezo mchezaji bora wa Afrika, Mbwana Samatta katika sherehe
zitakazofanyika Juni 4, 2016 kwenye kijiji cha Wasani Mwanzega Mkuranga.
Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim
Taalib alisema jana Dar es Salaam kuwa maandalizi ya sherehe hizo
itaambatana na ugawaji nyumba 31 kati ya hizo moja kubwa, tatu ndogo na
misingi 27 ya nyumba hivyo kufikisha jumla ya nyumba 150.
Alisema baba yake Mbwana Mzee
Ali Samatta amethibitisha kuwepo kwa mwanae katika sherehe hizo ambazo
naye ametunukiwa kuwa mwanachama wa heshima wa mtandao huo na kukubali
kushirikiana kuhakikisha michezo inakuwa nchini.
“Baba yake Samatt alisema
wakati akiwa kijana alikuwa mfungaji mzuri kwa timu alizowahi kuchezea
miaka ya sitini kama vile timu ya shele ya Sekondari ya Mzumbe, timu ya
mkoa wa Morogoro, timu ya Polisi na badaye aliwahi kuichezea Simba akiwa
na akina Hamisi Kilomoni” alisema Taalib.
Alisema sherehe hizo pia
zitapambwa na wasani kutoka vikundi mbalimbali vya ngoma na sarakasi
kutoka jijini Dar es Salaam na mkoa wa Pwani..
Alisema SHIWATA ilimzawadia
uanachama wa heshima mchezaji huyio baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji
bora wa Afrika na kutangaza kumpatia eneo la ekari tano kwa ajili ya
kujenga kituo cha wanamichezo.
0 maoni:
Chapisha Maoni