Jumatano, 11 Mei 2016

SHAKA HAMAD SHAKA:SEREKALI YATAKIWA KUAJIRI NA KUPELEKA WAGANGA ,WAUGUZI NA WAKUNGA KATIKA MAENEO YA VIJIJINI

Kaimu Katibu Mkuu Uvccm Taifa Shaka Hamdu Shaka Akizungumza Katika
Mkutano Ulio Fanyika Katika Ukumbi Wa Ccm Mkoani Tanga Lakini Pia Katika
Mazungumzo Yake Alimtaka ,Mstahiki Meya Kutopokea Hongo Za Wapinzani Ili
Kujiuzuru Alisema ”Mstahiki Meya Tunatambua Chama Cha Cuf Kinataka
Kukupa Hongo Ili Ujizuru Nafasi Hiyo Nnakutahadharisha Kamwe Usijaribu
Kukichezea Chama Cha Mapinduzi Na Sisi Kama Vijana Wa Ccm Tunakutaka
Kupuuza Yote Na Kufanya Kazi Bila Vishawishi Vyovyote Ili Tufikie
Malengo Ya Kuitekeleza Ilani Ya Ccm 2015-2020  Uchaguzi Umekwisha Sasa
Ni Muda Wa Kazi”
Wanachama Wapya Wakila kiapo cha Chama na Jumuiya
Na Woinde Shizza, TangaSerikaki umeshauriwa kusomesha , kuajiri na kupeleka waganga, wauguzi na
wakunga katika maeneo ya vijijini ili ukokoa maisha ya kina mama
wajawazito, iiiweko kutoa huduma bora za afya na tiba . Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi  (UVCCM )umetoa ushauri huo baada
ya ujumbe wa Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo  kutembelea hospitali kuu ya
Bombo katika Manispaa ya Mji wa Tanga.
Kaimu Katibu Mkuu Shaka Hamdu Shaka alitoa ushauri huo  alipomaliza
kutembelea hospitali hiyo , kusikiliza kero , kupata maelezo toka kwa
muuguzi wa zamu Atose  Kiluvia katika hospitali ya Bombo mkoani hapa .
Shaka aliueleza Muuguzi Kiluvia amueleze mganga mkuu wa wilaya kwamba  
ili kufikia malengo ya mil enia kuna ulazima wa kuhakikisha  maisha ya
kina mama wajawazito yanawekewa utaratibu bora wa kudumu ili  kunusuru
maisha yao , kupata ushauri wa maendeleo yao nyakati za ujauzito
wakipata huduma katika vituo vya huduma ya  afya.
Alisema ili huduma hizo ziweze kuimarika na kutolewa kwa wakati, mkakati
pekee ujaohitajika na kupewa kipaumbele ni kuweka mazingira bora
kuanzia halmahsuri za wilaya hadi serikali kuu ili kusomesha, kuajiri na
kupeleka wakunga, waganga na wauguzi maeneo ya vijijini.
“Mikakati ya maendeleo ya uimarishaji  huduma za msingi za kijamii
ziibuliwe katika ngazi za halalmshauri za wilaya kabla ya Serikali kuu
haijaweka mkono wake, madiwani na wakurugenzi wa halmashauri watenge
muda wankushughulikia nw kuondosha kero mapema” alishauri Shaka.
Alisema haiwezekani madiwani wakashiriki  vikao vya Baraza la madiwani
ambalo ni bunge la wilaya bila kujadili huduma zznjamii lama vike ujenzi
wa vituo vya afya, masuala ya kilimo, mifugo, miundombinu au ajira za
wakunga, waganga na wauguzi.
Aidha alisema haiwezekani kuzungumzia mpango wa maendeleo ya nchi huku
kukiwa na hali ya kuzorota kwa huduma za jamii kama tiba , chanjo na
kinga au kuwepo  upungufu wa wauguzi, wakunga na waganga .
“Zijengwe nyumba bora za kisasa ambazo waganga, wakunga na wauguzi
wataishi na kuridhika, walimu na wataalam wengine wa maendeleo ya kiseta
pia wawe na nyumba za uhakika maeneo ya vijijini. “Alisema
Halmashauri ikipeleka umeme, zikajengwa barabara, nyunba za wataalam
wetu , hakuna atakayekataa kuishi vijijini, siasa ya ujamaa na
kujitegemea haina maana watu  waishi katika nyunba za nyasi, hata
mkienga  nyumba  za roshani bado mtabaki kuwa wajamaa.
Alisema serikali kuu haiwezi kufanya kila kitu katika vitongoji, vijiji,
kata na kwenye  wilaya,kazi hiyo lazima ifanywe na halmashauri zetu
wakiwemo wataalam na madiwani.
“Kazi ya serikali kuu ni kupeleka  ruzuku, fedha za ruzuku zisitafunwe
na mchwa , kazi ya madiwani ni  usimamizi wa matumizi bora ya fedha za
umma, yakipatikana mafanikio  kila kijiji ndiyo maendeleo ya Taifa
“alisema Shaka ambaye emeanza ziara ya siku sita mkoani hapa.

0 maoni:

Chapisha Maoni