Jumatano, 11 Mei 2016

JUMLA YA SILAHA 36 ZAZUILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI ARUSHA





Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo

Na Woinde Shizza,Arusha
Kufuatia  zoezi la kuhakiki  silaha linaloendelea  hapa nchini jeshi la polisi mkoani Arusha  limefanikiwa
kuhakiki jumla ya silaha 2640  na  jumla ya silaha 36 zilizosalimishwa
zimefutiwa leseni za umiliki kutokana na sababu mbalimbali .
Akiongelea swala hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema kuwa
silaha  silaha hizo zimebaki chini ya uangalizi wa jeshi la polisi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo na baadhi ya
wamiliki kupitisha umri wa kumiliki silaha  ,wengine wakiwa wagonjwa  pamoja na wengine kukosa sifa ya kumiliki silaha
hizo.
Alisema kuwa umri wa kumiliki silaha mwisho ni miaka 70  ambapo kuna baadhi ya wananchi ambao walikuwa wanamiliki silaha hizo tayari wameshafikia ukomo wa umri wa kumiliki silaha hizo kisheria.
Aidha alisema pia kuna baadhi ya watu ambao walikuwa wanamiliki silaha zaidi ya moja bila sababu yeyote nao wamenyang’anywa huku wengine wakiwa wamechukuwa silaha hizo bila kujua matumizi halali ya umiliki wa silaha hizo.
Alitaja aina ya silaha ya silaha mbalimbali ambazo  tayari
zimekaguliwa na kukabidhiwa kwa wamiliki kuwa ni  bastola 1434,Raifo 540 pamoja na Shortigun 666.
Alisema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea kuhakiki silaha hizo hivyo wananchi wote ambao wanamiliki silaha wajitokeze na silaha zao kwa ajili ya kuhakikiwa kwani zoezi likiisha wataanza upekuzi wa silaha zote ambazo hazijahakikiwa na mtu akikutwa nayo akiwa ajahakiki ataokana ametenda kosa la kumiliki silaha kinyume cha sheria
Mkumbo pia aliwasihi watu wote ambao wanataka kumiliki silaha kwenda kupata mafunzo kwanza
kabla ya kukabidhiwa silaha na ambaye amesahamu matumizi ya silaha basi arudi  kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi
juu ya matumizi sahihi ya silaha.
wanamiliki silaha wajitokeze na silaha zao kwa ajili ya kuhakikiwa kwani zoezi likiisha wataanza upekuzi wa silaha zote ambazo hazijahakikiwa na mtu akikutwa nayo akiwa ajahakiki ataokana ametenda kosa la kumiliki silaha kinyume cha
sheria .
Mkumbo pia aliwasihi watu wote ambao wanataka kumiliki silaha kwenda kupata mafunzo kwanza kabla ya kukabidhiwa silaha na ambaye amesahamu matumizi ya silaha basi arudi  kwa ajili ya mafunzo ya muda mfupi juu ya matumizi sahihi ya silaha.

0 maoni:

Chapisha Maoni