JESHI la polisi Mkoa wa Pwani
linamshikilia Frowin Mbale (26) ambaye ni mkazi wa kawe Jijini Dar es
Salaam kwa tuhuma za kufanya mauaji ya kikatili ya mke pamoja na
mtoto wake kwa kuwachinja shingoni na kisu kasha kuwatupa vichakani.
Akizungumza na mwandishi wa
habari hizi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Boniventura Mushongi
amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kudai kuwa tukio hilo limetokea
jana majira ya saa 10:30 jioni katika kijiji cha zinga kata ya Dunda
Wilayani Bagamoyo.
Kamanda Mushongi amebainisha
kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na mwenzake mmoja aliyejulikana kwa jina
la Rajabu Juma (20) na walifanikiwa kuwakamata jana usiku majira ya saa
2:30 katika maeneo ya kijiji cha zinga.
Pia Kamanda Mushongi amewataja
marehemu hao kuwa ni Oliver Erasto (200 pamoja na mwanae Emmanuel Frowin
(3) ambao miili yao ilikutwa imetupwa katika vichaka vya kaole kata ya
dunda
“Kutokana na tukio hili
watuhumiwa wote kwa sasa tumewashikiria baada ya kutaka kutoroka ila kwa
bahati nzuri wananchi waliweza kutoa taarifa mapema kwa vyombo
vinavyohusika na ndipo walipofanikiwa kuwakamata,”aisema Kamanda
Mushongi.
Aidha alifafafnua kuwa
mtuhumiwa huyo akiwa na rafiki yake walimlaghai mkewe waongozane pamoja
wakiwa na mototo wao kwenda kuangalia ujenzi wa nyumba yao unaoendelea
katika eneo la kaole lakini walipofika huko ndipo walipoamua kufanya
tukio la mauaji hayo ya kikatili.
Mushongi akielezea zaidi
kuhusiana na tukio hilo amesema uchunguzi walioufanya umebaini mauji
hayo yametokana na wivu wa mapenzi, ambapo mume huyo alikuwa
akimtuhumu mke wake kuwa na mahusiano wa kimapenzi na mtu mwingine
aliyejulikaana na kwa jina la moja la Hamza mkazi wa kawe.
Katika hatua nyingine Mushongi
amelaani vikali tabia kama hiyo na kuwataka wazazi na walezi Mkoani
Pwani kutovunja sheria kwa kujichukulia sheria mikononi kwani kufanya
hivyo ni kinyume cha taratibu na sheri za nchi.
0 maoni:
Chapisha Maoni