Alhamisi, 5 Mei 2016

MIKANDA YA UBINGWA WA DUNIA WATAKAYOGOMBANIA MASHALI NA CHEKA YAWASILI NCHINI

Mratibu wa mpambano wa ungingwa wa Dunia wa U.B.O Anton Rutta katikati akionesha mikanda ya ubingwa watakayogombania mabondia Cosmas Cheka atakaecheza na Fransic Kimani wa Kenya na Thomasi Mashali kulia akiwa na mkanda wa ubingwa wa Dunia atakaocheza na Sajjad Mehrab kutoka ‘Irani’ mpambano utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa siku ya mei 14 Picha na SUPER D BOXING NEWS
……………………………………………………………………………………………………………………..
 Na Mwandishi Wetu
HOMA ya mpambano wa kimataifa imezidi kupamba mota baada ya leo kukutanishwa mabondia wote  wa Tanzania watakaocheza na mabondia wa  nje na kuongea na wahandishi wa habari  baada ya kuwasili kwa mikanda ya ubingwa wa Dunia itakayogombaniwa na mabondia wawili wa Tanzania
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mratibu wa mpambano huo Anton Rutta amesema mabondia wote wapo safi kwa ajili ya mpambano huo wa kimataifa, ambapo bondia Thomas Mashali ‘Simba Asiyefugika’ atakuwa anagombea ubingwa wa dunia Kg 76 mkanda wa U.B.O na Sajjad Mehrab kutoka ‘Irani’
huku Cosmas Cheka atakuwa akigombania ubingwa wa Dunia  wa U.B.O uzito wa Super Fether Kg.59  dhidi ya mkenya Fransic Kimani
  Wakati mapambano mengine ya kimataifa yatawakutanisha mabondia 
  Mwanadada Lulu Kayage atakaezichapa na Chiedza Homakoma ‘Nikita’ wa Malawi  wengine ni Ramadhan Shauri atakaepambana na Osgood Kayuni wa Malawi wakati Twaha Kassim atapambana na Fred Nyakese kutoka Kenya na Saleh Mkalekwa atakumbana na James Onyango wa Kenya huku  Francis Miyeyusho akivaana na Frank Kiwalabye wa Uganda
Katika mapambano mengine  Nassibu Ramadhani atacheza na Edward Kakembo wa Uganda Abdalla Pazi ‘Dula Mbabe’ atavaana na  Chamunorwa Gonorenda kutoka Zimbabwe mapambano mengine ya kitaifa yatawakutanisha  Shaban Kaoneka atakaecheza na Hassan Mwakinyo na Issa Nampepeche atakumbana na Baina Mazola mapambano hayo ya kimataifa yameandaliwa na promota mkongwe Ally Mwazowa kutoka mkoa wa Tanga

0 maoni:

Chapisha Maoni