Jumapili, 15 Mei 2016

TATIZO LA MADAWATI LAMALIZIKA SHULE YA MSINGI ULONGE,IRINGA


WADAU wa maendeleomkoani Iringa  wametakiwa kuendelea kujitolea katika zoezi la kuchangia  madawati  katika shule zenye uhaba  ili kumaliza tatizo hilo mashuleni.

Akizungmza wakati wa kuakbidhi madawati 30 yenye thamani ya Tsh.1,800000katika shule ya msingi Ulonga ilipo kata ya Igumbilo Manispaa ya Iringa mkoani hapa,kikabidhi  kwa niaba ya Suahil Thakore,Hamza Gangi alisema msaada huo umetokana na mkoa wa Iringa kuwa na upungufu wa madawati,,hivyo wao kama wadau wa maendeleo wameguswa kutoa mchango huo ili kupunguza kero ya uhaba wa madawati shuleni hapo.

Ginga alisema  kutokana na kilio cha serikali kupitia mkuu wa mkoa Amina Masenza kuhamasisha wadau wa Elimu kuchangia katika sekta hiyo,kwa nia ya kuiunga mkono serikali kwa juhudi kubwa inazofanya kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zilizopo.
Kutokana na omba la mkuu wa mkoa na kuona umuhimu wa watoto kusoma katika mazingira mazuri tumeona tuiunge mkono serikali.Ninawaomba wadau wenzangu kuitikia kwa wingi kumuunga mkono mkuu wa mkoa na serikali kwa ujumla’’’’’’alisema

Alisema ni jambo la kusikitisha na kushangaza kuona watoto kukaa zaidi ya wawili katika dawati moja wakati mkoa wetu una rasilimali ya misit,pamoja na hayo tunapaswa kuchangia,Tushikamane kwa pamoja  kila mmoja ili tuweze kuondoa kero hii ukizingatia wanaoumia ni watoto shule ambao wanasoma katika mazingira magumu.

Akipokea msaada huo kwa niaba ya mkurugenzi wa Manispa ya Iringa,Afisa Elimu Msinga Haji Mnasi alisema serikali pekee haiwezi kutosheleza hitaji la madawati,hivyo kila mawanachi  mmoja mmoja na wadau wa maendeleo kulingana na nafasi yzao wanapaswa kuliangalia hili kwa jicho pevu.

Alimshukuru Suhail kwa mchango wake na kuwataka wadau wengine kujitokeza kujitolea  bila kuchoka  na kusema kuwa kwa upande wa Elimu msingi manisapaa inakabiliwa uhaba wa nyumba za walimu katika shule mbalimbali na vyoo kwa wanafunzi.
‘’’Ili wanafunzi waweze kujifunza vizuri mazingira yanatakiwa yaboreshwe ikiwemo vyoo na ,madawati,madarasa na walimu,hivyo wadau wanahitajika ili kuhakikisha tunashirikiana kukabilianan na hizo changamoto ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri’’’’’’alisema’’’’’’
Maurice Mwilapwa ni mkuu wa shule ya Ulonga iliyopata msaada huo nae alimshukuru madau wa Elimu kwa kutambua uhitaji wa madawati katika shule hiyo ,ambapo alisema kuwa jumla ya watoto 60 watakaa katika madawati hayo.
.
‘’’’’’’’’Shule nzima inajumla ya wanafunzi 491,uhitaji wa madawati 184,    kulikuwa na upungufu wa madawati 37 ,baada ya kutolewa 30 yamebaki madawati 7 ambapo  6 yapo kwenye ukarabati kutoakana na ubovu, ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi waliopo,ambapo wanafunzi kuanzi darasa la kwanza hadi la tano wanakaa watatu katika dawati moja na darasa la sita na saba wanakaa wawili katika dawati moja ni dhahiri kwamba tulikuwa na upungufu mkubwa,tunamshukuru Suhail kwa mchango wake’’’’’’alisema
Aidha alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa walimu,nyumba za walimu, na matundu ya vyoo ambapo kwa sasa walimu waliopo  ni 9 na hitaji lake ni walimu 13,hivyo walimu wanaotakiwa kuongezeka ni8 ili kuleta uwiano na wanafunzi..

‘’’’’’Tunahitaji nyumba 17 za walimu kutokana idadi ya walimu waliopo na tuna nyumba moja tu,hali hii inasababisha walimu kufanya kazi katika mazingira magumu na hatarishi kutokanan na kuaka umbali wa eneo la kazi,hivyo naiomba serikali iweze kufikilia kwa kina kwa kusahirikianan na wadau tuweze ktatua changamoto hii’’’alisema
‘’’’’’’Uhaba wa vyoo ni tatizo kubwa kwa wananfunzi kiafya kutokanan na matundu yaliyopo kuwa mabovu hali inayohatarisha usalamam mdogo kiafya kwa wanafunzi wetu.matundu yanayohitajika ni 10 ya kisasa haya yaliyopo ni 12 ya kizamani na hayakidhi mahitaji ya wanafunzi kutokanan na idadi kubwa iliyopo’’’’’’ alisema





0 maoni:

Chapisha Maoni