Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob mapema leo Mei 5.2016
ametangaza kuwasimamisha kazi kwa watumishi wawili wa Manispaa ya
Kinondoni, akiweo Mwanasheria Mkuu BW. Burton Mahenge na Mthamini wa
Manispaa Bw. Einhard Chidaga baada ya Madiwani kuamua kwa kauli moja
kuwachukulia hatua hiyo.
Akisoma
taarifa na nyaraka mbalimbali mbele ya wanahabari, Mh. Boniface Jacob
alieleza kuwa: Kikao cha Kamati ya fedha na Uongozi cha tarehe
29/04/2016, kiliagiza kuwa yaorodheshwe mashauri yote ambayo
hayakusimamiwa vizuri na Mwanasheria wa Manispaa Bwana Burton Mahenge,
na hivyo kuisababishia Manispaa kupata hasara, kupoteza mali, na
kuchelewa kupata manufaa katika mali zake.
“Kufuatia
makosa yaliyogundulika katika mashauri hayo, baraza la Madiwani la
terehe 04/05/2016, limeamua kuwasimamisha kazi Mwanasheria Mkuu wa
Manispaa Bw. Burton Mahenge, na Mthamini wa Manispaa Bw. Einhard
Chidaga”.
Mh. Boniface Jacob aliyataja Makosa yaliyogundulika katika Mashauri hayo ni kama yafuatayo:-
- Mradi wa uwekezaji wa Oysterbay Villa. Mkataba huo, ulifanyiwa marekebisho mbalimbali bila idhini ya Halmashauri na hali hiyo kumpatia sauti zaidi Mwekezaji na kuamua analotaka. Manispaa ilipaswa kupata shilingi milioni 900 kwa mwaka katika uwekezaji huo,lakini kutokana na Mgogoro wa kimkataba mapato hayo hayajawahi kulipwa hivyo kupoteza shilingi billion 4.5 mpaka sasa. Mradi ulikamilika tangu 2011 katika viwanja vyote viwili kiwanja Na.277 na 322 ambapo uwekezaji katika kiwanja namba 277 una nyumba (Apartments) 44 na katika kiwanja Na.322 nyumba 68 (Mwekezaji nyumba 29 KMC Nyumba 17)
2 .Mgogoro wa wapangaji wa Nyumba za Magomeni Kota.
Manispaa
iliandaa mpango wa kuendeleza eneo la Magomeni Kota , hivyo kuwaondoa
wapangaji hao na kubomoa nyumba hizo kongwe. Wapangaji walifungua shauri
la kupinga kuondolewa katika nyumba, na kutoa madai ya kujengewa
nyumba,ama
kulipwa fedha za fidia kutokana na usimamizi hafifu wa shauri hili
Mahakama imeruhusu iliamuru Manispaa kukaana kumalizana na wapangaji nje
ya mahakama. Halmashauri ikatengeneza mkataba wa kuwalipa wapangaji
kiasi cha shilingi 1,080,000/= kwa kila mpangaji kama kodi ya Mwaka na
kumpatia kila mpangaji kiwanja.Hivyo Manispaa inatakiwa kulipa shilingi
3,271,520,000/= kugharamia fidia hiyo,kwa mchanganuo wa
Tshs.695,520,000/= pango la mwaka na Tsh2,576,000,000/=fidia ya viwanja
644.
3.Uwekezaji Eneo la Coco Beach Oysterbay.
Manispaa
iliingia Mkataba wa Q-Consult Limited. Kampuni hiyo ilishindwa
kutekeleza mradi kwa wakati na Manispaa ikavunja Mkataba huo. Q-consult
Limited ilifungua shauri ambalo halikusimamiwa vizuri na kwa sababu ya
kutofika kwenye kesi, Manispaa ilipoteza kesi hiyo. Halmashauri
iliagiza kukata kwa rufaa lakini hakukuwa na hatua zozote
zilizochukuliwa, na hivyo Manispaa inaweza kupoteza haki yake. Iliagizwa
na serikali mwanasheria mkuu baada ya tamko la Rais Mhe. John Pombe
Magufuli kutangaza nia ya kutoachia eneo hilo mpaka sasa mwanasheria
alikuwa hajakata rufaa.
4.Mradi wa ujenzi wa maduka Makumbusho (Eastern Capital LTD)
Katika
shauri hili mabadiliko ya mradi yalifanyika bila idhini ya Halmashauri
kwa kubadili michoro na kuongeza maeneo mengine katika mradi kama vile
kituo cha Mabasi , Matangazo na choo. viwango vya mgawanyo wa mapato ya
Manispaa katika maeneo yaalioongezewa ni kidogo ukilinganisha na
uhalisia.
Halmashauri
haina mkataba na mwekezaji kwa baadhi ya uendeshaji wa majengo ‘above
two storey’hazipo kwenye kumbukumbu za Halmashauri.
Mkataba
juu ya ujenzi na uendeshaji wa stendi hauna manufaa kwa Halmashauri
,KMC inapata 1%ya makusanyo kwa mwaka sawa na mil.4 tu kwa mwezi wakati
kabla ya uwekezaji ,local standy Halmashauri ilikuwa ikipata 12mil. kwa
mwezi.
5.Kubomolewa Kwa Ofisi ya Kata ya Msasani.
Mwanachi
aliyejulikana kwa jina la Chacha aliingilia eneo la Ofisi ya Kata
Msasani na baadae kuishitaki Manispaa.Usimamizi dhaifu wa shauri hilo
ulisababisha mahakama kutoa amri ya kubomoa ofisi ya Kata, Manispaa
imekata rufaa na sasa ni muda mrefu shauri halisikilizwi na hakuna
ufuatiliaji unaoendelea. Hata hivyo bwana Chacha kwa makusudi aliamua
kuuza kiwanja hiki, kwa Lake Oil Co. Limited wakati shauri halijaisha.
Manispaa imekosa manufaa mengi kwa kuchelewa kukamilika kwa shauri
hilo.Tangu upandewa pili ulikataa jaji.Tuna zaidi ya mwaka hatuja
pangiwa jaji mwingine na hatujafuatilia kama Halmashauri.
6.Ujenzi wa Nyumba za Makazi. (Apartments ) Hill Road Oysterbay
Mradi
unafanyika kwa ubia na Mwekezaji Texas Enterprise company LTD, Mkataba
uliingiwa mwaka 2009, na Mradi umesimama kwa Muda Mrefu sasa.
Pamefanyika
mabadiliko katika Mkataba na Mkataba umefanyiwa marekebisho bila idhini
ya Halmashauri. Manispaa inakosa manufaa ya Mali yake kwa sababu ya
kuchelewa kwa Mradi. Lakini pia uendeshaji mpya wa sasa hauna
makubaliano wa Financial proposal na Investment capital.
- Ujenzi wa nyumba za Makazi(Apartments).Kiwanja Na. 314 Toure Drive.
Mradi
huu unatekelezwa kwa ubia na Kampuni ya Lake Oil Limited. Mkataba
uliingiwa 2019. Mabadiliko yamefanyika katika Mkataba bila Idhini ya
Halmashauri na kusababisha Mradi kuchelewa kukamilika. Manispaa inakosa
Manufaa ya Mali yake kwa kuchelewa kukamilika mradi huu.
Aidha,
Mh. Boniface Jacob amesema kuwa, itakuwa ni jambo la aibu kwa Manispaa
kushindwa kuchukua hatua suala la mradi wa Coco Beach, licha ya Rais
Dk. John Pombe Magufuli kutaka eneo hilo libaki kuwa mali ya wananchi na
si kumuachia mwekezaji kuweka miradi yake.
Hata
hivyo Mwanasheria huyo wa Manispaa hakuweza kuchukua hatua yoyote hadi
sasa hivyo kuonekana bado mchezo unachezwa hivyo maamuzi ya kusimamishwa
ambapo pia licha ya kusimamishwa, Meya huyo amebainisha kuwa,
atachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria kwa mamlaka husika za
Kiserikali.
Tazama MO tv, kuona tukio hilo hapa:
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob akizungumza na wanahabari
mapema leo wakati wa kutoa tamko hilo la kuwasimamisha viongozi hao
akiwemo Mwanasheria Mkuu wa Manispaa. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagulumjuli.
Meya
wa Manispaa ya Kinondoni, Mh. Boniface Jacob akionyesha moja ya nyaraka
za Manispaa hiyo zilizokuwa zikichakachuliwa na watumishi hao
Mkutano huo ukiendelea
Diwani
kwa tiketi ya Chadema, Bi. Rose Moshi akizungumza wakati wa mkutano huo
ambapo ameeleza kuwa, Madiwani wote bila kuangalia chama wanatakiwa
kuchukua hatua pamoja na kuungana ilikotokomeza ubadhilifu wa mali za
Umma ilikusaidaia wananchi waliowachagua.Diwani Mteule wa Kata ya Kunduchi kwa tiketi ya CCM Michael Urio
akizungumza katika mkutano huo na wanahabari ambapo ameunga mkono
juhudi za Meya huyo wa Manispaa ya Kinondoni kwa hatua yake ya kuchukua
hatua kwa watendaji wazembe.
Waandishi
wa Habari wakifuatilia mkutano huo wakati wa Meya akitoa tamko la
kuwasimamisha watumishi mapema leo Mei 5.2016 katika ukumbi wa Mikutano
wa Manispaa. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog)
0 maoni:
Chapisha Maoni