TIB
Corporate Bank imefadhili mkutano mkuu wa bodi ya usajili wa
wakandarasi nchini unaotarajiwa kufanyika jijini Mwanza kwenye hoteli ya
Malaika kuanzia tarehe 5 hadi 6 mwezi huu wa tano ikifuatiwa na mkutano
mwingine utakaofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Daimond
Jubilee kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa tano.
Mkutano
huo, ambao mwaka huu una kauli mbiu ya ‘Kuwajengea Uwezo Wakandarasi wa
Ndani kwa ajili ya Uchumi Endelevu: Changamoto na Mipango ya baadae?,
unalenga kuwakutanisha wadau na wakandarasi kujadili mchango wa
wakandarasi na ushiriki wao katika kukuza uchumi wa nchi.
Akizungumzia
udhamini wa katika mkutano huo, Mkurugenzi wa TIB Corporate Bank, Bwana
Frank Nyabundege alisema benki yake inazifahamu changamoto
zinazowakabili wakandarasi wengi nchini ikiwemo ukosefu wa fedha ambao
unazuia kupanua na kuendeleza uwezo wao wa kushindana katika sekta ya
ujenzi hasa katika kupata zabuni na utekelezaji wa mikataba.
TIB
Corporate Bank imeweka misingi ya kuhakikisha inatoa huduma bora kwa
wateja wake na ndio maana tumeweza kuja na suhulisho kwa ajili ya
kuwasaidia wakandarasi kuweza kuendesha shughuli zao kwenye mazingira
yao ya kazi’ alisema Bw.Nyabundege.
Bwana
Nyabundege pia alisema udhamini wa mkutano wa wakandarasi unalenga
kujenga na kuimarisha uwezo wa wakandarasi kupata fursa ya kuendeleza
sekta ya ujenzi nchini.
TIB
Corporate Bank ilianzishwa kwa lengo la kutoa huduma za nyongeza za
kibenki kama mtaji wa kufanyia kazi, mikopo pamoja na uwezeshaji wa
kibiashara kwa ajili ya wateja mbalimbali kupitia ubunifu wa teknolojia,
kukuza thamani kwa wadau na pia kuchangia katika ujenzi wa taifa kwa
kutoa huduma mtambuka za kifedha na kuchangia ukuaji wa uchumi shindani
sambamba na Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025.
TIB
imefanya mabadiliko ya kitaasisi ili kuweza kuwa kituo cha huduma zote
za kifedha kwa kushughulikia mahitaji ya wawekezaji wa ndani wote kwa
lengo la kusukuma maendeleo ya uchumi wa taifa.
0 maoni:
Chapisha Maoni