Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) juu ya tuzo ya kimataifa ya viwango iliyotolewa
na International Federation of Purchasing and Supply Manangement(IFPSM)
kwa bodi hiyo hivi karibuni kulia ni mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey
Mbanyi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akionesha kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) vitabu vya mtaala mpya wa mafunzo ulioanza na Bodi ya
wataalamu ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB)Desemba mwaka 2015 kulia ni
mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey Mbanyi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha akionesha kwa waandishi wa habari
(hawapo pichani) tuzo ya viwango vya kimataifa kutoka International
Federation of Purchasing and Supply Manangement(IFPSM) iliyotolewa kwa
bodi hiyo hivi karibuni kulia ni mkurugenzi wa mafunzo Bw. Godfrey
Mbanyi.
……………………………………………………………………………………………………………….
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Bodi ya wataalam wa manunuzi na
ugavi (PSPTB) imetunukiwa tuzo ya viwango vya kitaalamu vya kimataifa na
International Federation of Purchasing and Supply Manangement(IFPSM) na
kutambulika rasmi kimataifa kwa kuwa na vigezo vya utoaji huduma katika
viwango vya kimataifa.
Katika taarifa iliyotolewa na
Afisa Masoko na Mahusiano mwandamizi wa (PSPTB)Bi Shamim Mdee imesema
tuzo hiyo ilitolewa kwa PSPTB mwezi Februari mwaka 2016 na kuifanya
PSPTB kuwa bodi ya kwanza barani Afrika kupata tuzo hiyo ya viwango vya
kimataifa kutoka IFPSM.
Taarifa hiyo imesema kuwa
upatikanaji wa tuzo hiyo ni matunda ya ushirikiano kati ya watendaji na
Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Bw. Clemence Tesha katika kuiendesha bodi
hiyo kufanikisha malengo na mipango yake katika utendaji kazi.
Mara baada ya PSPTB kupata tuzo
hiyo Rais wa IFPSM Dkt Paul Davi kwa niaba ya Bodi ya wataalamu wa
viwango vya kimataifa ameipongeza PSPTB kwa kazi kubwa walioifanya na
kuwa taasisi ya kwanza Barani Afrika kufikia kiwango cha kutambulika
kimataifa kwenye taaluma hiyo.
Kabla ya kupata tuzo hiyo, PSPTB
ilikuwa mwanachama muhusishwa wa IFPSM tangu mwaka 2015 lakini kutokana
na utendaji wa kazi wake, Bodi ya viwango ya kimataifa ikawatunuku tuzo
ya kuwa na viwango vya kimataifa katika utoaji wa taaluma hiyo Barani
Afrika kwa ujumla.
Aidha ,taarifa hiyo imesema kuwa
PSPTB imezindua mtaala mpya wa mafunzo tangu Desemba mwaka 2015 na
mtaala huo kwa sasa unaendelea kufundishwa katika vituo mbalimbali vya
maandalizi ya mitihani ya Bodi ambapo mtihani wa kwanza chini ya mtaala
mpya utafanyika November 2016.
Taarifa imeeleza kuwa umuhimu wa
mtaala huo ni pamoja na utaratibu wa kuanzisha masomo ya usimamizi wa
manunuzi wa umma kuanzia ngazi za chini hadi juu na pia utaratibu huu
utawataka watahiniwa kufaulu ngazi yoyote ya mtihani ndani ya miezi 24
toka kufanyika kwa mtihani husika kwa mara ya kwanza.
Katika kuzingatia utoaji wa
taaluma ya manunuzi na ugavi nchini Bodi ya wataalamu wa manunuzi na
ugavi itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya
nchi ili kusaidiana na kupambana na changamoto zilizopo katika kupeleka
mbele gurudumu la taaluma hiyo.
0 maoni:
Chapisha Maoni